Nyimbo Mpya: Rapa Joh Makini Aachia Ngoma Mpya ‘Brand’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa mashuhuri Joh Makini amezidi kuweka historia kwenye muziki wa Hiphop nchini Tanzania baada ya kuachia ngoma mpya yenye jina ‘Brand’ kwenye mitandao ya kutiririsha muziki.

Kwenye ‘Brand’,  Joh Makini anatumia mtindo wa tamaduni Hip-hop katika kuwasilisha ujumbe wake. Huu ni wimbo ambao Joh anatoa ushauri kwa wanamuziki wengine kuwa wasidharau wasanii wakongwe ambao wameshuka kimuziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond ‘Unachezaje’, Harmonize ‘Serious Love’ na Ngoma Zingine Zinazotamba Tanzania Wiki Hii

Pia anawaonya wasanii juu ya hulka yao ya kudharau mashabiki pindi wanapopata umaarufu na mengine mengi.

"Kudharau zile brand kubwa zilizoanguka ni kuwavunja moyo wachanga wanaoinuka. Local ila kikazi wanastahili kuheshimika backstage hazina ulinzi wanapita tu kama kaunta, ukisikia sound nzuri ujue ni mgeni sio wa hapa tunapokezana mic kama mbio za vijiti,” anaimba Joh kwenye aya ya pili.

Soma Pia: Joh Makini Akana Kusaidiwa na Meneja wa Diamond Kupata Collabo na AKA

Ngoma hii ya ‘Brand’ imeachiliwa kwenye mitandao ya kutiririsha muziki ikiwa ni takribani mwezi mmoja tangu msanii huyo kutokea kundi la Weusi aachie ngoma yake ya ‘Swagg’ ambayo ameshirikiana na Nandy.

Ngoma hii imetayarishwa na Hermy B kutoka studio za B Hitz. Hermy ana wasifu wa kufanya kazi na wasanii wakubwa kutokea nchini Tanzania kama M Rap, Mabeste, Gosby pamoja na Vanessa Mdee kupitia ngoma yake ya ‘Closer’ ambayo ilimtambulisha vyema kwenye muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=ufHogQDsYD4

Leave your comment