Nyimbo Mpya: Diamond ‘Unachezaje’, Harmonize ‘Serious Love’ na Ngoma Zingine Zinazotamba Tanzania Wiki Hii

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tukiwa tunaikamilisha wiki ya kwanza ya mwaka 2022, tasnia ya muziki nchini Tanzania imezidi kunoga hasa kwenye mtandao ambako wasanii wengi sana hupendelea kupakia ngoma zao.

Soma Pia: Matukio 5 ya Kimuziki Yanayotarajiwa Kutikisa Bongo Mwaka wa 2022

Zifuatazo ni ngoma tano ambazo zinafanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa nchini Tanzania:

Unachezaje - Diamond Platnumz

Diamond Platnumz ameendeleza ubabe wake kwenye mtandao wa YouTube baada ya ngoma yake ya ‘Unachezaje’ iliyotayarishwa na S2kizzy kuendelea kufanya vizuri YouTube. Kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 2.8 kwenye mtandao huo.

https://www.youtube.com/watch?v=Y8n1qpw7Ijw

Soma Pia: Zuchu Adokeza Tarehe Atakayoachia Video Ya 'Kitu'

Why - The Ben ft Diamond Platnumz

‘Why’ ni ngoma ambayo imekonga hisia za wana Afrika Mashariki wote kwani ukiweka, kando video ya ngoma hii kuwa na hadhi ya kimataifa, pia matumizi ya lugha takriban tatu kwenye ngoma hii yamechagiza ngoma hii kufanya vizuri sana.Kufikia sasa imeshatazamwa takriban mara Milioni 1.3 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=10tGnm2h9qQ

Serious Love – Harmonize

Video ya tatu kutoka kwenye albamu yake ya ‘High School’, bila shaka ‘Serious Love’ ni video ambayo imependwa sana na mashabiki. Video hiyo imebeba maudhui yaliyoshibana sana na mashahiri ya ngoma yenyewe. Kufikia sasa ngoma hio imeshatazamwa mara laki tano tisini na tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=59jN0K1n7ZM

Kitu - Zuchu ft Bontle Smith & Tyler ICU

Kupitia Amapiano hii, Zuchu amedhihirisha uwezo wake wa kuimba aina tofauti tofauti ya muziki na ndio maana kazi hii imepokelewa kwa ukubwa sana na mashabiki. Kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 1 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=tLnn97BDy9g

Hunijui - Nay Wa Mitego

Kwenye ‘Hunijui’,  Nay Wa Mitego anaponda na kuwatumia ujumbe watu ambao wanafatilia sana maisha yake. Video ya wimbo huu imezidi kunogesha kazi hii kutokana na kuwa na stori ya kuchekesha ambayo imeakisi maisha ya miaka ya zamani. Kufikia sasa imeshatazamwa mara laki sita hamsini na mbili kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=7hxMHUqihd4

Leave your comment