Matukio 5 ya Kimuziki Yanayotarajiwa Kutikisa Bongo Mwaka wa 2022

[Picha: Tuko]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwaka 2021 ulikuwa ni mwaka ambao ulisheheni matukio mengi yaliyopamba tasnia ya muziki nchini Tanzania. Kuanzia utambulisho wa Mac Voice, Ali Kiba kuachia albamu na Diamond Platnumz kuwania BET, bila shaka 2021 ulikuwa ni mwaka ulioweka alama kubwa kwenye Bongo Fleva. Lakini vipi kuhusu 2022, ni matukio gani ambayo yanatarajiwa kutikisa kwa mwaka huu?

Soma Pia: Wasanii 5 wa Bongo Wanaotarajiwa Kuachia Albamu Mwaka 2022

Yafuatayo ni matukio matano ya kimuziki yanayotarajiwa kuzua gumzo kwa mwaka 2022.

Albamu ya Diamond Platnumz

Hakuna shabiki wa muziki wa Bongo Fleva asiyefahamu kuwa Diamond Platnumz yupo mbioni kuachia albamu yake. Taarifa kutoka kwa msanii huyo inaaashiria kuwa albamu hiyo inatarajiwa kuwa na ngoma 12 tu huku wengi wakishuku kuwa wasanii wengi wa kimataifa huenda wakashiriki kwenye mradi huo.

Kurudi kwa tuzo za muziki nchini Tanzania

Baada ya ukimya wa takribani miaka sita bila Tanzania kuwa na tuzo za muziki, ilipofika mwezi Mei mwaka 2021 Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Innocent Bashungwa alitangaza kurejeshwa kwa tuzo za muziki nchini humo mwishoni mwa mwezi Desemba 2021. Na pamoja na kwamba tuzo hizo hazikufanyika mwezi Desemba kama ilivyoahidiwa , wadau wa muziki wameshuku kuwa ndani ya mwaka 2022 tuzo hizo zinatarajiwa kurudi kwa kishindo.

Soma Pia: Wasanii Kutoka Tanzania Wanaotazamwa Zaidi Kwa Mwaka 2022

Tamasha la Afro East Carnival la Harmonize

Itakapofika Februari 14 mwaka 2022, Harmonize ametangaza kufanya tamasha lake kubwa la Afro East Carnival kwemye mojawapo ya viwanja vikubwa vya matamasha hapa jijini Dar Ea Salaam. Tamasha hili linatarajiwa kuwa kubwa sana kwani itakuwa kwa mara ya kwanza Harmonize anatumbuiza kwenye tamasha lake mwenyewe la uwanjani. Kupitia tangazo lake la instastory, aliahidi kushirikisha wasanii wakubwa wa hapa Afrika Mashariki.

Wasanii kuanza kulipwa mirabaha kutoka kwenye vituo vya Redio

Baada ya mwezi Juni mwaka 2021, Rais Samia kutangaza kuwa wasanii wataanza kulipwa mirabaha mwishoni mwaka huo bado zoezi hilo halijakamilishwa na mamlaka ya COSOTA ambayo ndio inahusika katika utaratibu mzima wa malipo na bila shaka ndani ya mwaka 2022 zoezi hilo linatarajiwa kukamilika na wasanii wa Tanzania kuanza kulipwa kwa kadri nyimbo zao zinavyochezwa kwenye vituo vya Redio.

Msanii mpya kutambulishwa Next Level Music

Kwa sasa macho na masikio yapo kwa msanii Rayvanny ambaye ndani ya mwaka huu anatarajiwa kutambulisha msanii mpya kwenye lebo hiyo ya Next Level Music ambayo kwa sasa inatamba na wasanii wawili ambao ni Rayvanny na Mac Voice.

Leave your comment

Top stories

More News