Joh Makini Akana Kusaidiwa na Meneja wa Diamond Kupata Collabo na AKA

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutokea nchini Tanzania Joh Makini amekanusha madai ya Sallam SK ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz pamoja na Zuchu kuwa alimsaidia kupata collabo yake na AKA kwenye ngoma ya ‘Don't Bother’.

Kupitia kipindi cha Dizzim TV cha kuitwa The Joint ambacho Sallam SK pia ni mtangazaji, siku chache zilizopita meneja huyo alifunguka kuwa alimsaidia Joh Makini kupata collabo hiyo na AKA ili kukamilisha ngoma ya hiyo ya ‘Dont Bother’.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny na Harmonize Waongoza Orodha ya Wasanii Wenye Wafuatiliaji Wengi Zaidi YouTube Afrika

Kwa mujibu wa Sallam, alifanya hivyo bila malipo yoyote. Baada ya kupata taarifa hizo, Joh Makini alitumia akaunti yake Twitter kukanusha kauli hiyo kutoka kwa Sallam SK huku akidokeza kuwa kuna baadhi ya wadau wa muziki walikuwa wanafanya hila ili asiweze kukamilisha collabo hiyo na AKA kutokea Afrika kusini.

"Yeye sio chanzo cha hiyo collabo. Mwarabu alipambana sana kukwamisha hii ni basi tu Mwenyezi Mungu hajawahi kushindwa," aliandika Joh Makini kupitia akaunti yake ya Twitter.

Joh Makini alizidi kudokeza kwa kuandika "Kwa mazingira niliyofanya collabo na AKA nitawashukuru sana Nikki Wa Pili na G Nako Warawara lakini waliomleta walikuwa hawataki itokee."

Soma Pia: Sallam SK Azungumzia Uhaba Wa Usimamizi Mzuri wa Wasanii Tanzania

Ngoma ya ‘Don't Bother’ iliingia sokoni mwaka 2015 na kuweza kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania. Ngoma hio ilitayarishwa na Nahreel kutokea The Industry huku video ya ngoma hiyo ilifanyika huko Afrika Kusini chini ya Justin Campos.

Leave your comment