Diamond, Rayvanny na Harmonize Waongoza Orodha ya Wasanii Wenye Wafuatiliaji Wengi Zaidi YouTube Afrika

[Picha: The Standard]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Muziki wa nchini Tanzania umeendelea kushika kasi barani Afrika na mtandao wa YouTube umezidi kudhihirisha hilo baada ya wasanii watatu kutoka Tanzania kuibuka vinara wa kuwa na wafuatiliaji (subscribers) wengi zaidi kwenye mtandao huo barani Afrika.

Ifuatayo ni orodha ya wasanii watano kutoka barani Afrika ambao wana wafuatiliaji wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Wasanii 5 wa Bongo Wanaotarajiwa Kuachia Albamu Mwaka 2022

Diamond Platnumz

Kutoka lebo ya WCB, Diamond Platnumz ndiye msanii kutoka barani Afrika anayeongoza kuwa na wafuatiliaji wengi zaidi YouTube. Diamond ana zaidi ya wafuasi Milioni 6 tangu ajiunge na mtandao huo mwaka 2011.

Rayvanny

Kufikia sasa Rayvanny ana wafuatiliaji takriban Milioni 3.4 kwenye mtandao wa YouTube. Yeye ndiye msanii wa pili kutoka barani Afrika kwa wafuatiliaji wengi huku video yake ya ’Tetema’ ikiwa ndio inaongozwa kwa kutazamwa kwenye akaunti yake, kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 62.

Harmonize

Hata baada ya kuondoka WCB, Harmonize ameendelea kuonesha cheche zake kwenye mtandao wa YouTube. Kufikia sasa ana wafuasi Milioni 2.9 kwenye mtandao huo hivyo kushika nafasi ya tatu huku video yake ya ‘Kwangaru’ iliyotazamwa mara Milioni 88 ikiwa ndio video iliyotazamwa zaidi kwenye akaunti yake ya YouTube.

Soma Pia: Bifu Tano Kubwa Kwenye Bongo Fleva Mwaka 2021

Davido

Kutokea nchini Nigeria, Davido anashika nafasi ya nne akiwa na wafuatiliaji takriban Milioni 2.82 kwenye akaunti yake ya YouTube. Ngoma yake ya ‘Fall’ imetazamwa mara Milioni 227 na ndio ngoma ya pili iliyotazamwa zaidi YouTube kwa nchini Nigeria.

Fally Ipupa

Kutokea nchini Congo, Fally Ipupa anashikilia namba tano akiwa na wafuatiliaji Milioni 2.66 na hivyo kumfanya kuwa msanii kutokea Congo mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao wa YouTube. Wasanii wengine kwenye kwenye orodha hiyo ni pamoja na Mr Flavour, Ckay, Burna Boy, Wizkid na Tekno.

Leave your comment