Sallam SK Azungumzia Uhaba Wa Usimamizi Mzuri wa Wasanii Tanzania

[Picha: Sallam SK Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Sallam SK, ambaye ni meneja wa msanii nyota Diamond Platnumz, amedai kuwa kuna uhaba wa usimamizi mzuri wa wasanii kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania.

Sallam aliweka wazi kauli hiyo kupitia chapisho aliloliweka mtandaoni. Kwa mujibu wa Sallam, Tanzania iko na wasanii wenye vipaji vya kuimba ila wanaathirika vibaya kutokana na usimamizi wao.

Soma Pia: Wasanii Kutoka Tanzania Wanaotazamwa Zaidi Kwa Mwaka 2022

Suala lingine ambalo linaathiri ukuaji wa muziki wa Tanzania kulingana na Sallam SK, ni elimu kwa wasanii ili wafahamu umuhimu wa kuwa na usimamizi unaolewa muziki vizuri.

Alieleza kuwa yafaa kuwe na makubaliano na kuelewana baina ya watu mbali mbali kwenye usimamizi wa msanii ili wanapofanya maamuzi wafanye kwa pamoja kama timu.

Aliendeleza ujumbe wake kwa kusema pia kuna ukosefu wa sheria za kuwalinda wawekezaji kwenye tasnia ya muziki.

Soma Pia: Diamond, Rayvanny na Harmonize Waongoza Orodha ya Wasanii Wenye Wafuatiliaji Wengi Zaidi YouTube Afrika

"Tanzania Ina wasanii wengi wazuri tu, kuna uhaba wa management Inayojua muziki, elimu kwa wasanii kujua umuhimu wa management, na sheria inayomlinda investor, muhimu kila mtu kujua jukumu lake na maamuzi yawe ya team sio ya mtu mmoia," Sallam SK aliandika mtandaoni.

Sallam SK ni mmoja kati ya wasimamizi wa wasanii ambao wanaheshimika mno Afrika Mashariki. Kazi yake nzuri kwenye usimamizi inadhihirika kupitia msanii wake Diamond Platnumz ambaye amepanda ngazi na kuwa msanii anayeheshimika duniani.

Leave your comment