AY Azungumzia Muziki wa Amapiano Kupata Umaarufu Tanzania
19 January 2022
[Picha: Wikipedia]
Mwandishi: Brian Sikulu
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Nyota wa muziki wa Hip-hop AY ametoa kauli yake kuhusu mjadala wa muziki wa Amapiano kupata umaarufu mkubwa nchini Tanzania.
Kwa siku za hivi karibuni, mjadala mkubwa umeibuka kuhusu mada hiyo huku baadhi ya washika dau kwenye tasnia ya muziki wakidai kuwa umaarufu wa Amapiano umefifisha muziki wa bongo, ambao ndio kitambulisho cha muziki wa Tanzania.
Soma Pia: Hamisa Mobetto Adokeza Ujio wa Kolabo Zake na Otile Brown, Bien
AY ambaye pia ni mmoja kati ya wasanii wakongwe zaidi Tanzania, amechangia kwenye mjadala huo. Kupitia ukurasa wake wa kijamii, AY alidai kuwa huenda walioshiriki kwenye muziki wa Amapiano wakaambulia patupu kimapato.
Msanii huyo alisema kuwa watanzania wanaohusika kwenye muziki wa Amapiano hawapati hela kama vile wasanii wa Afrika Kusini.
"Wakuu, Wasanii na Ma Dj's waliokuwa busy na kufanya Amapiano hapa Tanzania...mpaka Leo Nani kashaenda South Africa kuokota hela zao tujifunze biashara?" AY aliandika mtandaoni.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Tommy Flavour Aachia Ngoma Mbili Mpya ‘Lay Down’ na ‘Kidogo
"Maana naona wasanii na dj's wa South Africa wanavyokuja kuokota hela Bongo, Nini shida?" aliendeleza ujumbe wake.
Baadhi ya wasanii wakubwa kutoka Tanzania wamefanya muziki wa Amapiano na kazi zao zimepokelewa vizuri sana. Kuna wasanii wengine hata hivyo wamepinga muziki huo na kuapa kuwa kamwe hawataufanya.
Hivi maajuzi, malkia wa muziki wa bongo Zuchu alilazimika kujibu tuhuma kuwa muziki wa Bongo umekufa kutokana na Amapiano. Kwa mujibu wa Zuchu, wasanii wanaofanya Amapiano wanazidisha ustadi wao katika midundo tofauti.
Leave your comment