Hamisa Mobetto Adokeza Ujio wa Kolabo Zake na Otile Brown, Bien

[Picha: Hamisa Mobetto]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamitindo Hamisa Mobetto, ambaye pia ni msanii kutoka Tanzania, amedokeza ujio wa kolabo baina yake na wasanii wakubwa wa Kenya. Hamisa Mobetto kwa sasa yupo nchini Kenya kwa shughuli ya kuchangisha pesa ya kusaidia watoto mayatima.

Kwenye kikao na wanahabari, Hamisa aliulizwa iwapo anapanga kufanya kazi na wasanii wa Kenya. Alisema kuwa tayari ako na kolabo na wasanii nyota Otile Brown pamoja na Bien kutoka Sauti Sol.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny ft. Zuchu ‘I Miss You’ na Ngoma Zingine Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

Hii itakuwa mara ya kwanza Hamisa Mobetto kushirikiana na wasanii wa Kenya. Wasanii hao wawili waliotajwa, hata hivyo, si wageni kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania, kwani wametoa kolabo na wasanii wa bongo.

Bien kupitia bendi la Sauti Sol amefanya kazi na Nandy, huku Otile Brown akiwa amefanya kazi na Alikiba pamoja na Harmonize. Kwa mujibu wa Hamisa, kolabo hizo zipo tayari na kilichosalia ni kuziachia tu.

"I have a song with Otile Brown, kolabo hizo zipo tayari na kilichosalia ni kuziachia tu. Tulishafanya iko tayari, tutatoa. I also have a song with Bien," Hamisa Mobetto alisema.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Tommy Flavour Aachia Ngoma Mbili Mpya ‘Lay Down’ na ‘Kidogo’

Msanii huyo hata hivyo hakutoa tarehe kamili ambazo nyimbo hizo zitatoka au maudhui yake. Kolabo hizo zinatarajiwa kumpandisha Hamisa Mobetto cheo kwenye tasnia ya muziki na kumpa mashabiki hata zaidi kutoka Kenya.

Leave your comment