Nyimbo Mpya: Rayvanny ft. Zuchu ‘I Miss You’ na Ngoma Zingine Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

[Picha: EA Feed]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwaka 2022 unazidi kusonga na bila shaka wanamuziki kutoka Tanzania wamezidi kupamba mwaka huu kwa kuachia kazi mpya ambazo zinazidi kupeperusha bendera ya muziki wa Bongo Fleva. Ndani ya wiki ya pili ya mwezi Januari, zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka kwa wasanii wa Tanzania:

Soma Pia:  Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia ‘I Miss You’ Akimshirikisha Zuchu

I miss you - Rayvanny ft Zuchu

Baada ya ‘Number One’ kufanya vizuri, Rayvanny amesherehesha watanzania na ngoma yake ya mpya ya ‘I miss you’ ambayo amemshirikisha Zuchu. ‘I Miss You’ ni ngoma ya mapenzi ambayo kuanzia ujumbe mpaka midondoko yake itakukosha.

https://www.youtube.com/watch?v=T69CmY6Kc5g

Chetu - Billnass

Kama unatafuta ngoma yenye mdundo wenye nguvu na ambayo itakupa faraja na tumaini hasa kwenye kipindi ambacho umekata tama, basi huna budi kuitegea sikio ‘Chetu’ kutoka kwa Billnass, ngoma ambayo ni ya kwanza kwa Billnass kwa mwaka 2022.

https://www.youtube.com/watch?v=1MtpJ7_NDtU

Who - Platform

Wiki hii Platform alizidi kuwaaminisha watanzania kuwa hata bila collabo na Ruby, bado anaweza kufanya vizuri. Kwenye ‘Who’, Platform analilia mapenzi kwani mtu anayempenda sio mwaminifu kwenye mahusiano.

https://www.youtube.com/watch?v=vm9HWj3vYTY

Baibui - Ally Nipishe

Ally Nipishe anarudi tena kwenye uwanja wa Bongo Fleva na ngoma yake ya ‘Baibui’ ambayo kwa sasa ndio habari ya mjini hapa Tanzania. Nipishe ambaye anasifika kwa sauti na uandishi mujarab kwenye kazi hii anamuimbia mwanamke ambaye si mwaminifu kwenye mapenzi lakini anatumia vazi la baibui na upole wake kulaghai wanaume.

https://www.youtube.com/watch?v=N1LJOYLyFew

Tausi - Mrisho Mpoto & Mbosso

Muingiliano wa kimashahiri, midondoko na hata mipangilio ya sauti kati ya Mbosso na Mrisho Mpoto kwenye ‘Tausi’ ni kitu cha kupigiwa makofi.

https://www.youtube.com/watch?v=T69CmY6Kc5g

Leave your comment