Nyimbo Mpya: Tommy Flavour Aachia Ngoma Mbili Mpya ‘Lay Down’ na ‘Kidogo’

[Picha: Nyimbo Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkali wa muziki wa RnB kutoka Tanzania Tommy Flavour ameweka tabasamu kwa mashabiki zake baada ya kuachia ngoma mbili mpya ambazo ni ‘Lay Down’ pamoja na ‘Kidogo’.

‘Lay Down’ ni ngoma ya RnB ambayo ndani yake Tommy Flavour anatuma ujumbe kwa mpenzi wake mpya kuwa atampenda na kumjali na kuahidi kuwa hatompiga wala kumdhalilisha mpenzi wake.

Soma Pia: Tommy Flavour Apinga Vikali Mahusiano Katili

Hii ni ngoma ambayo kwa mujibu wa Tommy Flavour inaakisi maisha ya kimahusiano ambayo alishawahi kupitia msanii huyo kwani kupitia chapisho lake la Instagram, Tommy alifafanua kuwa alishawahi kuwa mhanga wa kunyanyaswa kihisia kwenye mahusiano, kutukanwa na kutothaminiwa.

‘Lay Down’ imetayarishwa na Yogo Beats mtayarishaji wa muziki ambaye aghalab hufanya kazi na wasanii wa King's Music.

https://www.youtube.com/watch?v=rG0RCJjPLKw

Ngoma ya ‘Kidogo’ ni ngoma ambayo imechangamka zaidi kuanzia kwenye mdundo na midondoko mpaka kimashahiri. Ni ngoma ambayo inafaa hata kuchezwa kwenye klabu na sehemu za starehe.

Soma Pia: Tommy Flavour Azungumzia Kujipa Cheo cha Ufalme wa RnB

Hii ni ngoma ambayo Tommy anakiri namna ambavyo anampenda mwandani wake huku akituma ujumbe kwa watu wasiopenda mahusiano yao kuwa watasubiri sana ila yeye na mpenzi wake hawataachana.

‘Kidogo’ imetayarishwa na Blaq mtayarishaji wa muziki ambaye ameshafanya kazi na wasanii mashuhuri hapa Tanzania ikiwemo Zuchu na wengineo wengi.

https://www.youtube.com/watch?v=oe2-n9MtRdA

Leave your comment