Tommy Flavour Azungumzia Kujipa Cheo cha Ufalme wa RnB

[Picha: Afro Hits]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Tommy Flavour hivi karibuni amefunguka kuhusu chapisho la siku kadhaa zilizopita ambapo alitanabaisha kuwa kutokana nyimbo ambazo tayari ameshazirekodi, ni sahihi kabisa yeye kuitwa mfalme wa RnB.

Akizungumzia kuhusu chapisho hilo kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni kwenye kipindi cha XXL, Tommy alisema kuwa aliamua kujiita mfalme kwani anajiamini sana kutokana na muziki anaoufanya kuwa mzuri.

Read Also: Tommy Flavour Azungumzia Uwezekano wa Collabo na Zuchu

"Kujiita King sio katika hali ya ubaya lakini ni katika hali ya kujiamini katika kile ambacho nachokifanya kwa sababu naamimi katika kalamu yangu na nikiangalia kwa sasa hivi kwenye industry kwenye upande wa RnB tumekuwa sio wengi," alizungumza Tommy.

Tommy alizidi kuzungumza kwa kusema kuwa kwa sasa ubunifu kwenye muziki wa RnB umepungua sana tofauti na zamani ambapo wasanii wa RnB walikuwa na ubunifu mkubwa sana.

Read Also: Tommy Flavour Athibitisha Ommy Dimpoz Kuwepo Kwenye Album Yake Mpya

"Ubunifu umekuwa hamna kwa hiyo upande wangu mimi nimeona kutokana na kazi zangu nilizonazo. Mimi kings ambao nawajua ni kina Rama Dee, kina Steve kina TID huko nyuma walishine kama kings wa RnB lakini sasa hivi sioni king wa RnB sababu sioni mtu ambaye anashine kwenye RnB na kwa sasa hivi waliokuwepo sioni huo ubunifu," alizungumza Tommy Flavor.

Aidha, Tommy alitoa tahadhari kuwa, yeye kujiita mfalme wa RnB haimaanishi kuwa haeshimu wasanii wengine ambao wanafanya aina hiyo muziki.

"Pia ningependa kuweka sawa, sio kwamba najisikia au nataka kujigamba, hapana mimi sina hayo majigambo lakini ukizingatia mimi ni mtoto kutoka familia ya kifalme ni mtoto wa mfalme kutoka Kings music so kujiita mfalme katika sekta yangi si kitu kibaya," alitanabaisha Tommy.

Leave your comment