Tommy Flavour Azungumzia Uwezekano wa Collabo na Zuchu

[Picha: Bongo Swaggz]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tommy Flavour kwa sasa amekuwa ni kama keki ya taifa kutokana na ngoma yake ya ‘Jah Jah’ aliyomshirikisha Alikiba kufanya vizuri sana.

Katika mahojiano hivi karibuni, Tommy amesema kuwa yuko tayari kufanya collabo na Zuchu kama itatokea nafasi.

Soma Pia: Tommy Flavour Athibitisha Ommy Dimpoz Kuwepo Kwenye Album Yake Mpya

"Of course why not? Siku ikitokea kwa sababu napenda (Zuchu) anachokifanya," alisema Tommy.

 Hii ni habari njema kwenye muziki wa Bongo Fleva kwani lebo hizo mbili yaani WCB pamoja na Kings Music aghalab huwa kwenye ushindani wa kimuziki.

Kauli hii ya Tommy Flavour inaonesha kuwa utayari wa kufanya kazi baina ya lebo hizo mbili kubwa nchini Tanzania.

Aidha, Tommy Flavour alisema kuwa yeye na Zuchu wamekutana kama mara mbili tu huku mara ya mwisho kwa wasanii hao kukutana ilikuwa ni studio alipokuwa anarekodi ngoma yake ya ‘Omukwano’ aliyomshirikisha Alikiba.

Read Also: Tommy Flavour Awasifu Harmonize, Diamond Kwa Kupeperusha Bendera ya Tanzania Kimuziki

"Kipindi cha nyuma nafikiri marehemu mzee wake (Zuchu) alishawahi kumletaga studio kipindi hicho nafikiri alikuwaga mdogo mdogo kwa hiyo sikuwa nimemkumbuka sasa hivi. Baada ya kumuona yuko Wasafi ndo nikakukumbuka hiyo ndo ilikuwa siku narekodi Omukwano tulikuwa studio na siku ambao niliumuona mara ya mwisho," alizungumza Tommy Flavor.

Pamoja na kuwa lebo tofauti lakini wasanii wote wawili yaani Zuchu na Tommy Flavor wanafanya vizuri kwenye soko la muziki nchini Tanzania.

 Tommy Flavor kwa sasa yuko mbioni kuachia albamu yake ya ‘Heir To The Throne’ ambayo inasubiriwa kwa hamu.  

Leave your comment