Tommy Flavour Awasifu Harmonize, Diamond Kwa Kupeperusha Bendera ya Tanzania Kimuziki

[Picha: Tommy Flavour/Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii Tommy Flavour amewasifu Harmonize na Diamond Platnumz kwa juhudi zao za kupeperusha bendera ya Tanzania katika tasnia ya muziki.

Soma Pia: Tommy Flavor Afichua Sababu ya Kuandika Ngoma ya ‘Jah Jah’

Tommy Flavour alikuwa akizungumza baada ya kuulizwa kutoa kauli yake kuhusu wasanii hao wawili. Tommy Flavour alieleza kuwa wasanii hao wawili wanapigania kutambulisha taifa la Tanzania kimuziki.

 Tommy Flavour alipoulizwa kumchagua msanii mmoja kati ya hao wawili ambaye anapenda ufundi wake katika muziki, alishindwa kuchagua na kusema kuwa wote ni hodari ikija katika uandishi wa muziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Tommy Flavour Aachia ‘Jah Jah’ Akimshirikisha Alikiba

Msanii huyo alieleza kuwa anawapenda wasanii hao wote wawili katika nafasi tofauti huku akisistiza kuwa hawezi mchagua mmoja wao ilhali nguvu zao na njia zao katika muziki ni tofauti.

"Ni wasanii ambao wanalipigania taifa la Tanzania. Ni wasanii kama wasanii wengine wa Tanzania ambao wanafany vizuri na wanapigana kuitambulisha nchi yetu," Tommy Flavour alisema.

Akizungumzia suala la ubora katika uandishi wa ngoma, Tommy Flavour alisisitiza kuwa kwa sasa hafuatilii mitindo ya wasanii wengine. Kwa mujibu wa msanii huyo, yeye ako makini katika kuboresha muziki wake kwanza.

"Mimi kusema ukweli, mimi najiangalia sana zaidi ya mimi mwenyewe na watu ambao wananizunguka kwa sabaabu ndio focus yangu ilipo. Lakini sifuatili sana vitu vya watu wengine na kuanza ku judge," Tommy Flavour aliongeza.

Tommy alikiri kuwa yeye husikiliza ngoma za Diamond na Harmonize na huburudishwa na wote wawili.

Leave your comment