Tommy Flavor Afichua Sababu ya Kuandika Ngoma ya ‘Jah Jah’

[Picha:Yinga]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea lebo ya Kings Music Tommy Flavor ameeleza sababu ya kuja na wimbo wake wa Jah Jah ambao ameutoa hivi karibuni akimshirikisha AliKiba.

Kwenye ngoma hiyo, Tommy Flavour anasifu na kuutukuza ukuu wa Mungu na jinsi ambavyo Mungu amemvusha pale alipokuwa kwenye changamoto.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Tommy Flavour Aachia ‘Jah Jah’ Akimshirikisha Alikiba

Akiongea na kituo kimoja cha habari hapa nchini Tanzania, Tommy Flavour alisema kua aliamua kufanya ‘Jah Jah’ ambao ni muziki wa Injili ili kuwapa wafuasi wake kazi tofauti ni kile walichozoea.

"Wasanii inabidi tukue kimawazo kila siku kwa hiyo nikajaribu kufanya kitu tofauti kwa sababu nyimbo zipo nyingi kwenye albamu yangu kuna nyimbo za mpenzi, nyimbo nyingine kubang hivyo nikasema si mbaya nianze na hii kwa sababu nimepitia vitu vingi sana," aliongea Tommy Flavor.

Tommy pia alizidi kudokeza kuwa wimbo huo pia ni maalum kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa hapo alipofikia.

Soma Pia: Alikiba Atangaza Kukamilika kwa Albamu Yake

"Mpaka sasa hivi niko na mashabiki zangu na Mwenyezi Mungu nashukuru ameweza kunipa nafasi nyingine tena ya kufanya kitu katika sanaa hicho ni kitu kikubwa sana kwa hiyo nikaona si mbaya nianze na wimbo wa kumshukuru," alizungumza nyota huyo kutokea Kings Music.

Muda mfupi tu tangu ngoma hiyo kuingia sokoni, mashabiki wameweza kuipokea kwa ukubwa sana na mpaka sasa kwenye mtandao wa YouTube, imeshatazamwa mara laki nne elfu nne.

https://www.youtube.com/watch?v=IM0Rs05yiSw

Leave your comment