Alikiba Atangaza Kukamilika kwa Albamu Yake

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Staa wa muziki Alikiba hatimaye ametangaza kukamilika kwa albamu yake iliyosubiriwa kwa hamu sana na mashabiki wake.

Alikiba alichapisha tangazo hilo kwenye ukurasa wake wa Instagram wakati akiupigia kampeni wimbo mpya 'Jah Jah' kutoka kwa Tommy Flavour.

Soma Pia: Alikiba Apokea Tuzo Mbili Kutoka YouTube

Alikiba, hata hivyo, hakufichua habari zaidi kuhusiana na albamu yake ila aliwasihi wafuasi wake wawe wenye subira huku akijiandaa kuachia tangazo rasmi.

Msanii huyo hakufichua jina la albamu hiyo au idadi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu yake.

"Wakati tunaendelea kuenjoy #JahJah ya @tommyflavour …. I just wanna let you know, finally My Album Is Done. Hold your breath and wait for the big announcement," chapisho la Alikiba mtandaoni lilisomeka.

Albamu ya Alikiba imesubiriwa kwa hamu sana na mashabiki kwani ilichukua muda mwingi kabla ya kukamilika. Hapo awali, Alikiba alifichua kuwa albamu yake ilichelewa kwa sababu za kiufundi.

Soma Pia: Alikiba Afichua Sababu Kuu Iliyochelewesha Albamu Yake

"Hizo ni nyimbo ambazo nimezi introduce tu lakini zitakuwepo kwenye album vile vile. Album inatoka anytime from now. Kuna vitu zenye zime delay tu dakika za mwisho kwa sababu za mastering na nini. Soon hiyo album inatoka," Alikiba alisema katika mahojiano ya hapo awali.

Alikiba ni miongoni mwa wasanii wa kwanza kutangaza kukamilika kwa albamu yao kati ya wanamuziki wakubwa Tanzania waliokuwa wameashiria kutoa albamu. Baadhi ya wasanii wengine ambao pia wanasubiriwa kutoa albamu zao ni Harmonize na Diamond Platnumz.

Leave your comment