Alikiba Apokea Tuzo Mbili Kutoka YouTube

[Picha: Pulse Live]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Alikiba ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Kings Music, ameingia katika orodha ya wasanii waliotuzwa na kampuni ya YouTube kutona na idadi ya wafuasi walionao kwenye mtandao huo.

Alikiba alipokea tuzo mbili kwa pamoja, ya kwanza ikiwa ya kufikisha wafuasi laki moja na nyingine na ya pili ikiwa ya kufikisha wafuasi milioni moja.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii na Maua Sama, Rosa Ree, Beka Flavor na Wasanii Wengine

Alikiba kwenye akaunti yake ya YouTube ya kibinafsi kama mwanamuziki amefikisha takriban wafuasi milioni moja. Kwa upande mwingine, akaunti ya YouTube ya Kings Music imefikisha wafuasi takriban nusu milioni.

Alikiba pamoja na wasanii wengine waliosaniwa kwenye lebo hiyo mara kwa mara huchapisha video zao kwenye akaunti ya Kings Music.

Soma Pia: Rayvanny Amtambulisha Msanii wa Kwanza wa Next Level Music

Mtandao wa YouTube huchangia mno katika mafanikio ya wasanii haswaa katika kizazi kipya cha muziki. Kupitia mtandao wa YouTube, wasanii hupata kipato kutokana na kazi zao na vile vile kuweza kusambaza kazi hizo ili ziwafikie mashabiki wao.

Miongoni mwa wasanii wengine kutoka Tanzania waliofikisha zaidi ya wafuasi milioni moja kwenye mtandao wa YouTube ni pamoja na Diamond Platnumz, Harmonize, Lava Lava, Mbosso, Rayvanny na Zuchu.

Leave your comment