Bongo Flava Takeover: Factors Contributing to Success of Bongo Music in Kenya

[Image Source: Jambo News]

By Lydia M Joshua

Get Free Music Updates and Mixes on Telegram

Bongo Flava is arguably one of the biggest music genres in Kenya and East Africa at large. The genre incorporates; Indian, Hip-Hop, Taarab, Muziki wa Dansi, and Dancehall beats to create a groovy and soulful flavour. ‘Bongo Flava’ which translates to ‘Brain’ and ‘Flavour’ in English, sprouted in the 1980's due to America’s hip-hop influence on young Tanzanians who tried to imitate their favorite artists by rapping and jamming in Swahili.

Read Also: How Kenya Music Entertainment Shifted from Live Shows to Virtual Concerts Due to Covid-19

Eventually, the effect of the genre became so strong that the name ‘Bongo’ became the identity of Tanzanians. For many years, renowned old school Tanzanian artists including; Mr Nice, Z Anto, Mr. Blue, Marlaw, Matonya, Ray C, and modern Bongo Flava artists including; Diamond Platnumz, Ali Kiba, Rayvanny, Harmonize have continuously dropped Bongo Flava hits, which have enjoyed massive success in Kenya, with some enjoying massive airplay across various broadcast stations.

In addition to Tanzanian artists, several Kenyan artists including; Otile Brown, Bahati, Nadia, Arrowbwoy, Masauti, Jovial and many more, have also tapped in and released well-produced Bongo Flava songs which have been doing well. In this article, we will be reviewing some of the major factors which have contributed to the success of Bongo Music in Kenya:

Read Also: Road Trip Best Music Compilation Playlist: Kenyan Edition

Swahili Language

If you talk to a man in a language he understands, that goes to his head. If you talk to him in his language, that goes to his heart. Those are the words of the late legendary Nelson Mandela. Building on the words of Nelson Mandela, apart from Swahili being one of the official languages in Kenya, it is also integrated into the education system. This means that a big part of the Kenyan audience understands the message in most of the Bongo Flava songs since they are mostly in Swahili.

Similarities in Culture

Being neighbours, Kenyans and Tanzanians share a lot in regards to culture. Most of what appeals to them also appeals to us making their music relatable and acceptable to the Kenyan audience.  The nuances in the songs, as well as the intensity of the message is not lost because of the cultural similarities including beauty standards.

Read Also: Is Amapiano A Passing Cloud In The Kenyan Music Scene?

Poetry

Bongo artists are known and respected for their ability to write songs with great poetic lines. The level of poetry in most Bongo songs make the pieces easy to resonate with. A good example is Zuchu’s songs which always go viral in Kenya due to the deep message hidden underneath the well-crafted lines. Some of her songs that have done extremely well in the country include ‘Sukari’ and ‘Nyumba Ndogo’ which have lots of poetry in them. On the other hand, Mbosso is also big in Kenya because he goes heavy on poetry in his love songs.

Quality Production and Creative Marketing

Bongo Flava artists for example Diamond Platnumz, Rayvanny, Harmonize and AliKiba are currently taking the world by storm, with most of their success being attributed to quality production of their music and creative marketing. Diamond and his Wasafi crew have heavily invested in digital marketing, thus making the Wasafi brand very popular in and outside Tanzania. The same technique has been adopted by Konde Music Worlwide and Kings Music Records under the leadership of Harmonize and Alikiba respectively.

Bongo Flava Artists Adaptability to Popular Music 

The ability for Bongo artists to adapt to popular music trends in Kenya has also been a major factor in contributing to the genre’s success in Kenya. The artists are able to mix Bongo with any other genre including; Reggae, Rhumba, and Amapiano. In fact, recently there has been an influx of Bongo Flava artists dropping hot mashups of Amapiano and Bongo Flava songs which have been taking the country by storm. Some of those jams include; ‘Nimekuzoea’ by Nandy, ‘Iyo’ by Diamond ft Focalistic, Mapara A Jazz and Ntosh Gazi.

 

Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii na Maua Sama, Rosa Ree, Beka Flavor na Wasanii Wengine

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kiwanda cha muziki nchini Tanzania kimeendelea kustawi kwa kasi kutokana na ukweli kuwa wasanii wameendelea kuachia ngoma nzuri tena bila ya kupumzika kitu ambacho kimeendelea kuburudisha mashabiki. Kwenye nakala hii tunaangazia nyimbo mpya zilizoachiwa wiki hii:

Soma Pia: Rayvanny ‘Wanaweweseka’, Jux ‘Sina Neno’, Diamond ‘Naanzaje’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania

Kusah - Hapana

Baada ya kuachia ‘Cheusi’ mwezi mmoja nyuma, wiki hii mwanamuziki Kusah ameachia ngoma mpya kabisa yenye jina ‘Hapana’. Kwenye ngoma hii, Kusah anatoa ahadi kuwa hawezi kumuacha mpenzi wake kutokana na mapenzi motomoto wanayopeana na mwandani wake. Kibao hiki kimeandaliwa na Cukie Dady mtayarishaji muziki ambaye pia amehusika katika maandalizi ya albamu ya Rapcha hasa ngoma ya namba 6 inayoitwa ‘Nitajimwaga’ kwenye albamu hiyo.

https://www.youtube.com/watch?v=mJlBOK4MxQg

Maua Sama –Away ft Young Lunya

Baada ya kimya cha takriban miezi sita hatimaye wiki hii Maua Sama amerudi tena na mkwaju wake mpya kabisa unaoitwa ‘Away’. Kwenye wimbo huu,  amemshirikisha Young Lunya. ‘Away’ ni wimbo wa mapenzi amabapo Maua Sama anaelezea namna ambavyo ana shauku ya kukutana na mpenzi wake baada ya kutoka safarini, huku Lunya nae akipigilia msumari ujumbe wa Maua kwa kuonesha namna ambavyo anampenda na kumkubali mpenzi wake.

https://www.youtube.com/watch?v=U6c6EyXcoAs

 Sitaki - Dogo Janja

Akiwa anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa, rapa Dogo Janja aliamua kuwafurahisha watanzania kwa kuachia ngoma yake ya ‘Sitaki’. ‘Sitaki’ imetayarishwa na Jini X 66 huku video ikiwa imefanyika huko kwenye jiji la Dubai na huu ni wimbo ambao ni makhususi kwa watu ambao wanafurahi kuwepo kwenye mahusiano na wenza wao.

https://www.youtube.com/watch?v=qcAUCRixKEk

Kama Siwezi - Beka Flavor

Pamoja na kumpenda na kumpa kila alichonacho mpenzi wake, Beka Flavor kwenye ‘Kama Siwezi’ anaelezea maumivu aliyonayo baada ya kutendwa na mpenzi wake aliyemthamini sana. Ngoma hii imeweza kufanya vizuri hapa Tanzania na hii ni kazi ya mtayarishaji wa muziki nguli kutokea Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=3HLOSGCAuS0

Wana Wanywe Pombe – Rosa Ree

Ilipofika Septemba 15 mwaka huu, Rosa Ree aliamua kulipua spika za redio hapa Tanzania na ngoma yake mpya ya ‘Wana Wanywe Pombe’. Kwenye ngoma hii, Rosa Ree anachana akisifia na kutoa sifa za kemkem za pombe na bila shaka wale watu wanaopenda kunywa pombe ngoma hii imekuja muda muafaka kwa ajili ya kuwaburudisha.

https://www.youtube.com/watch?v=uPM56wZhU5s

Leave your comment