Rayvanny ‘Wanaweweseka’, Jux ‘Sina Neno’, Diamond ‘Naanzaje’ na Nyimbo Zingine Zinazovuma YouTube Tanzania

[Picha: Mtikiso Entertainment]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Tasnia ya ya muziki nchini Tanzania imeendelea kupokea ngoma kali kutoka kwa wanamuziki nchini humo. Kwa wiki hii kwenye mtandao wa YouTube, mambo yameendelea kupamba moto kwani nyimbo nyingi zimefanya vizuri. Hivyo basi, makala hii inaangazia ngoma tano kutoka Tanzania ambazo zimefanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa YouTube:

Soma Pia: Nyimbo Kali Zilizowahi Kutoka Mwezi Septemba [Video]

Naanzaje - Diamond Platnumz

Ngoma ya ‘Naanzaje’ imeendelea kushika kasi nchini Tanzania na kwa wiki ya pili mfululizo, imeshika namba moja kati ya video zilizotazamwa zaidi kwenye mtandao huo. Kufikia sasa, video ya ‘Naanzaje’ imeshatazamwa mara Milioni 5.4 kwenye YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=iKbW2EDs_mE

Wanaweweseka - Rayvanny

Chui kutokea mbuga ya Next Level Music ameendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Wanaweweseka’. Kwenye wimbo huu, Rayvanny ametoa nasaha kwa watu wasiopenda uhusiano kuwa watasubiri sana. Lizer Classic kutokea Wasafi Records amehusika katika kutengeneza ngoma hii huku Eris Mzava akiwa amehusika kuandaa video.

https://www.youtube.com/watch?v=M6WisT8ocUE

Sina Neno - Jux

Zimeshatimia siku tisa tangu Jux aachie ngoma yake ya ‘Sina Neno’ ambayo ilizua gumzo kuu kwenye mitandao ya kijamii kutokana na mashahiri yake. Kufikia sasa, ngoma hii imeshatazamwa mara laki nane hamsini na nane kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=QCtkOnnhOng

Soma Pia: Nyimbo Tano Kali Kutoka Kwa Rapa Dogo Janja

Rais wa Kitaa - Nay wa Mitego

Ngoma hii kutoka kwa Nay wa Mitego inazidi kudhihirisha kuwa rapa huyo ni ‘Rais wa Kitaa’ kutokana na namna ambavyo wananchi wameipokea kwa ukubwa. Namna ambavyo Nay Wa Mitego amegusia masuala ambayo watanzania wanayapitia kwenye maisha ya kila siku imevutia watu wengi zaidi kutazama na kurahani ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=0AEyaLhZR8E

Teacher - Harmonize

Mwalimu wa Amapiano kutokea Tanzania kwa siku 17 mfululizo ameendelea kukaa kwenye nafasi za juu kwenye mtandao wa YouTube. Hii ni kwa sababu wengi wamekubali kazi hii kutoka kwa Harmonize. Kufikia sasa, ‘Teacher’ ya Harmonize imeshatazamwa mara Milioni 4.1 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=mPVoKSc6LJo

Leave your comment