Nyimbo Kali Zilizowahi Kutoka Mwezi Septemba [Video]

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kama wewe ni mpenzi wa muziki mzuri basi ni vyema kufahamu Septemba ni mwezi ambao una maana kubwa sana kwenye muziki wa Tanzania. Hii ni kwa kuwa wanamuziki wengi huachia ngoma zenye uzito wa hali ya juu ndani ya mwezi huu.

Soma Pia: Diamond ‘Naanzaje’, Jux ‘Sina Neno’, Harmonize ‘Teacher’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii

Makala hii imelenga kukupitisha kwenye nyimbo tano ambazo ziliachiwa mwezi Septemba miaka kadhaa nyuma na zikafanya vizuri sana:

Yope Remix - Inno B ft Diamond Platnumz

Innos B kutokea nchini Congo pamoja na Diamond walishirikiana kwenye ngoma hii ambayo iliingia sokoni Septemba 7 mwaka 2019. Video ya ‘Yope Remix’ iliyoongozwa na Director Kenny imechangamka vilivyo ikimuonesha Innos B na Diamond Platnumz wakisakata dansi kisawasawa na hii ndio video ambayo inaongoza kutazamwa zaidi kwa nchini Tanzania kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 165 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=ebZ7Ng1okCg

Pacha Wangu - Rich Mavoko

Miaka saba nyuma mwanamuziki Rich Mavoko alichangamsha Tanzania na video ya wimbo wake ‘Pacha Wangu’ ambayo ilitoka Septemba 26 mwaka 2014. Mdundo mkali kutoka kwa Mazuu pamoja na video ya kali kutoka Adam Juma iliiweka kazi hii kwenye hadhi ya kimataifa na mpaka sasa ni moja kati ya nyimbo bora za muda wote kutoka kwa Rich Mavoko.

https://www.youtube.com/watch?v=nw59lY5hpF4

Cheche - Zuchu ft Diamond Platnumz

Umeshatimia mwaka mmoja tangu Zuchu na Diamond Platnumz wateme ‘Cheche’ kwa mashabiki zao. ‘Cheche’ ambayo ilitayarishwa kwa ushirikiano wa Mocco Genius pamoja na Lizer Classic ilimuweka Zuchu kwenye medani za muziki wa kimataifa kutokana na mdundo na mashairi yake kukosha watu wa nchi mbalimbali na kufikia imeshatazamwa mara Milioni 24.

https://www.youtube.com/watch?v=vyUslddxOpI

I Just Wanna Love You - Navy Kenzo

‘I just wanna love you’ ni kazi nzuri kutoka kwa Aika na Nahreel ambayo iliingia sokoni Septemba 27 2014 takriban miaka saba nyuma. Audio ya wimbo huu iliandaliwa na Nahreel huku Director Khalfan alihusika katika kutayarisha video. Kufikia sasa ngoma hii imeshatazamwa mara laki mbili arobaini na mbili kwenye mtandao wa Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=NIOg8nAUx8Q

Unaibiwa – Rayvanny

Rayvanny aliachia kazi hii mwaka 2017 Septemba 12 kisha siku mbili baadae alisindikiza na video ambayo ilifanyika Afrika Kusini pamoja na Dar es Salaam. Mashairi ya wimbo huu yanatoa ujumbe kwa wanaumwe kuwa wawe makini na wenza wao. Rayvanny ameweza kuweka utani ambao unamfanya mtu afurahi pale anaposikia ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=Pb3adebbryg

Leave your comment