Diamond ‘Naanzaje’, Jux ‘Sina Neno’, Harmonize ‘Teacher’ na Nyimbo Zingine Zinazotamba YouTube Tanzania Wiki Hii

[Picha: Get Muziki]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Uwanja wa muziki ni mpana sana kiasi cha kwamba kila shabiki anaweza kuchagua ni wimbo upi ambao yeye anapenda kuusikiliza. YouTube ni sehemu mojawapo ambayo mashabiki hupata fursa adhimu ya kusikiliza ngoma za wasanii wawapendao. Makala hii imelenga kukupitisha kwenye ngoma tano ambazo zinatamba sana YouTube kwa wiki hii:

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video ya ‘Wanaweweseka’

Naanzaje - Diamond Platnumz

Siku takriban tano zilizopita Tanzania nzima ilizima baada ya Diamond Platnumz kuachia video ya ‘Naanzaje’ ambayo iliweza kuweka rekodi ya kipekee baada ya kutazamwa mara laki moja ndani ya dakika 40 tu. Ufundi mkubwa wa Hanscana katika ujenzi wa video hii ndio umesababisha watu wengi kuipenda na kufikia sasa imeshatazamwa mara milioni tatu nukta mbili kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=iKbW2EDs_mE

Soma Pia: Collabo 5 Kali Baina ya Wasanii wa Tanzania na Uganda [Video]

Rais wa Kitaa - Nay wa Mitego

Kitendo cha Nay wa Mitego kuwasemea watanzania kwenye wimbo huu wa ‘Rais wa Kitaa’ kimelipa sana kwani watu wemgi wameonekana kuupenda na kuguswa nangoma hii.  Kufikia sasa, wimbo huu umeshatazamwa mara milioni moja nukta mbili kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=0AEyaLhZR8E

Teacher - Harmonize

Mwalimu mkuu wa Amapiano nchini Tanzania Harmonize ameendelea kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Teacher’. Kwenye wimbo huu, Harmonize ameongelea namna ambavyo yeye ni ‘noma’ kwenye muziki na namna ambavyo washindani kwenye muziki wanamuiga yeye. Mpaka sasa ‘Teacher’ imetazamwa mara milioni tatu nukta sita kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=mPVoKSc6LJo

Sina Neno - Jux

Kazi nzuri ya Bob Manecky pamoja na mashairi ya kubembeleza, yenye utulivu na ya kugusa kutoka kwa Jux bila shaka yamefanya kazi hii iwe bora sana. Kwenye ‘Sina Neno’, Jux anatoa pongezi kwa mpenzi wake kwa kupata ujauzito pia anaweka wazi kuwa hana tatizo lolote na mpenzi wake wa zamani badala yake anamtakia kheri na upendo kwenye maisha yake.

https://www.youtube.com/watch?v=QCtkOnnhOng

Ni wewe - Killy ft Harmonize

Wimbo wa ‘Ni wewe’ umeendelea kufanya vizuri sana kutokana na mashahiri mazuri yaliyoipamba pamoja na mdundo mkali uliopikwa na mtayarishaji wa muziki Hunter. Kufikia sasa, wimbo huu umeshatazamwa mara Laki nne sabini na sita kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=ixzllSyWSdU

Leave your comment