Nyimbo Mpya: Rayvanny Aachia Video ya ‘Wanaweweseka’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Nyota kutokea Next Level Music Rayvanny ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Wanaweweseka’.

Kwenye ‘Wanaweweseka’, Rayvanny ameamua kuua ndege wawili kwa wakati mmoja. Kwa upande mmoja, yanatoa sifa kedekede kwa mpenzi wake huku upande wa pili Rayvanny anatoa ujumbe kwa watu ambao wako kinyume na mahusiano yake kuwa watasubiri sana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Dully Sykes Aachia Ngoma Mpya ‘Biggie’

"Wenye wivu wasijinyonge ila wapigwe shoti wafe king'asti wangu yuko hapa usinishike bega niache," anaimba Rayvanny mwanzoni kabisa mwa wimbo huu ambao umepokelewa kwa mikono na mashabiki.

Rayvanny anaendeleza kumpa sifa mpenzi wake kwa kuimba "Presha inapanda Presha inashuka wanaovimba watapasuka. Nikiposti namba Insta itachafuka watatamani kuhack waje kufuta."

Lizer Classic kutokea Wasafi Records pamoja na Sound Boy ndio wamehusika kutayarisha wimbo huu.

Soma Pia: Collabo 5 Kali Baina ya Wasanii wa Tanzania na Uganda [Video]

Video ya ‘Wanaweweseka’ imezua gumzo zaidi kwani Paula Kajala ambaye ni mpenzi wa Rayvanny ametumika kama video vixen.

Video hii imeongozwa na Eris Mzava Director ambaye ameshafanya video nyingi sana na Rayvanny kama vile ‘Siri’, ‘Jeniffer Remix’, ‘Teamo’, ‘Chawa’ na nyinginezo nyingi ambazo zimefanya vizuri ndani na nje ya Tanzania.

Kufikia sasa, video ya wimbo huu imeshatazamwa mara laki mbili sitini na moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=M6WisT8ocUE

Leave your comment