Nyimbo Mpya: Dully Sykes Aachia Ngoma Mpya ‘Biggie’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki Dully Sykes kutokea nchini Tanzania amerudi tena kwenye kiwanda cha Bongo baada ya kuachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Biggie’.

Ndani ya wimbo huu, Dully Sykes ametumia sana lugha ya picha kujielezea namna ambavyo yeye anawapagawisha wanawake na kufanya wakimbie wanaume waluokuwa nao kwenye mahusiano ili wawe nae.

Soma Pia: Collabo 5 Kali Baina ya Wasanii wa Tanzania na Uganda [Video]

Bila shaka ukisikiliza wimbo huu utafahamu kuwa maneno ya tafsida yametumika sana ili kupunguza ukali wa ujumbe ulioko kwenye mistari yake Dully Sykes.

"Hii kitu ndefu kama treni ya zigi inawafanya watoto wazuri wasotaka kucheat wanacheat wanahaha kama digidigi yani wanakuja spidi sarakasi na misamba kama ya gigi. Washakutana nazo ila vijana hawana ligi wamedata na yangu coz ya kwangu iko bigi bigi," anaimba Dully Sykes kwenye aya ya kwanza.

Wimbo huu umetayarishwa na nguli wa muziki Tanzania Mr T Touch kutokea Touch Sounds na ambaye ameshiriki kuandaa ngoma za wasanii wengi kama Nay Wa Mitego, Billnass, Diana Nyange, G Nako na wengine wengi.

Soma Pia: Ommy Dimpoz Adokeza Ujio wa Kolabo Yake na Nandy

Huu ni wimbo wa tatu kutoka kwa Dully Sykes kwa mwaka huu kwani Februari mwaka huu aliachia ‘Mtaa wa Ngoto’ kisha akaachia ‘Nancy’ mwezi unaofuatia wa Machi.

https://www.youtube.com/watch?v=_iYkz24E04w

Leave your comment