Ommy Dimpoz Adokeza Ujio wa Kolabo Yake na Nandy

[Picha: Southern TZ Forum]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Ommy Dimpoz amedokeza ujio wa kolabo nyingine baina yake na malkia wa muziki wa bongo Nandy.

Ommy Dimpoz aliweka wazi taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram. Ommy Dimpoz hata hivyo hakufichua habari zaidi kuhusiana na kolabo hiyo kando na uwepo wake. Hakueleza tarehe kamili ya uzinduzi wa ngoma hiyo wala jina ambayo ngoma hiyo itapewa.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Juma Jux Aachia ‘Sina Neno’

Ommy Dimpoz kupitia chapisho hilo pia alimshukuru Nandy kwa kumualika katika tamasha lake la Nandy Festival lililofanyika mkoani Dar es Salaam. Ommy alionekana mwingi wa furaha kwa kuweza kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

Alikiri kuwa alikua na hamu sana kuitambulisha kolabo yake na Nandy ila mashabiki watasubiri kidogo kabla ya kupakuliwa ngoma hiyo.

"Thank You @officialnandy for having me last night…. it was epic. We got Another Anthem Coming Soon I can’t wait," chapisho la Ommy Dimpoz mtandaoni lilisomeka.

Hii itakuwa ngoma ya pili ambayo Ommy Dimpoz atakuwa anashirikiana na Nandy. Ngoma ya kwanza ambayo wawili hao walishiriakiana ilipewa jina la 'Kata'. Ngoma hiyo ilitolewa mapema mwaka jana kwa mfumo halisi na pia kwa mfumo wa remix.

Soma Pia: Ngoma ya Harmonize ya 'Fall In Love' Yachezwa BET

'Kata' ilipokelewa vizuri sana na mashabiki na hata kutazamwa mara mingi sana kwenye mtandao wa YouTube. Video halisi ya wimbo wa ''Kata'' kufikia sasa imetazamwa mara milioni tano nukta tatu huku remix yake ikiwa na watazamaji milioni moja nukta moja.

Ommy na Nandy ni miongoni mwa wasanii wenye ushawishi mkubwa sana nchini Tanzania na bila shaka kolabo yao inasubiriwa kwa hamu sana.

Leave your comment