Nyimbo Mpya: Juma Jux Aachia ‘Sina Neno’

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Juma Jux ameachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Sina Neno’.

Jux ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa chapa yake ya African Boy ameachia wimbo huo ambao ameimba kwa hisia sana.

Soma Pia: Jux Azungumzia Kufanya Kazi na Megan Thee Stallion

Kwenye wimbo huo, msanii huyo amesisitiza kuwa hana ugomvi na mpenzi wake wa zamani ambaye ni mjamzito na badala yake anamtakia heri na fanaka kwenye mahusiano yake mapya.

Wengi wametafsiri wimbo huu kama ujumbe wa Jux kwa mpenzi wake wa zamani Vanessa Mdee ambaye siku ya jana alipamba vichwa vya habari ulimwenguni baada ya kutangaza kuwa ni mjamzito.

"Sikuchukii nakuombea maisha mema maisha mema ya furaha Mungu aoneshe njia. Si nimezoea ila nina furaha kuiona familia. Niko salama mimi sina neno utaitwa mama mtoto mpe upendo," anaimba Jux kwenye aya ya kwanza.

Watu wengi mtandaoni wameonekana kuguswa sana na wimbo huu na hata katika ukurasa wa YouTube wa Jux, mashabiki wengi wameonekana kuleta mrejesho chanya na wamemsifia Jux kwa kuwapa wimbo bora.

Mtayarishaji wa wimbo huu wa kwanza ni Foxmadeit pamoja na nguli wa muziki Bob Manecky ambaye ameshafanya kazi na Jux kwa miaka 14 na pia ameshafanya kazi na wanamuziki wengine kama Killy, Quick Rocka na wengineo.

https://www.youtube.com/watch?v=QCtkOnnhOng

Leave your comment