Jux Azungumzia Kufanya Kazi na Megan Thee Stallion

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea Tanzania Juma Jux amezungumzia kufanya kazi na rapa kutokea nchini Marekani Megan Thee Stalion. Jux ameweka wazi kuwa hana mawasiliano yoyote na rapa huyo na wala hawana wimbo wa pamoja.

Kauli hii ya Jux imeweka sawa hali ya sintofahamu iliyokuwepo baina ya mashabiki ambao walishuku kuwa wasanii hao wawili wana wimbo wa pamoja baada ya Megan Thee Stalion kuonekana akicheza wimbo wa Jux wa ‘Mapepe’ Februari mwaka huu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Jux Zinazovuma 2021

Baada ya kuona video hiyo, Jux alimtakia Megan Thee Stalion heri ya kumbukizi ya kuzaliwa na aliwasihi mashabiki kuendeleza kumtag Megan Thee Stallion ili kuwepo na remix ya wimbo huo wa ‘Mapepe’.

Ila mpaka sasa, Megan Thee Stallion hajajibu chochote.

Akiongea kwenye mahojiano yake na Lil Ommy Jux amesema : "Siwezi kudanganya sikuwahi kuwa na mahusiano yoyote naye (Megan Thee Stallion) na hata before mwenyewe nilikuwa surprised kama watu wengine."

Aidha Jux alifichua kuwa kama Megan Thee Stallion atajibu ujumbe wake huko kwenye mtandao wa Instagram basi bila shaka msanii huyo atatumia fursa hiyo kuomba collabo na msanii huyo.

Soma Pia: Stamina Aweka Wazi Tarehe na Jina la Albamu Yake Mpya

"Im a fan napenda muziki wake sana of course mi ni mfanyabiashara so tutajua tunafanyaje lakini she is a big artist nafasi kama hiyo kama itapatikana why not tutajaribu kuona inafanyika vipi," alidokeza Jux.

 Aidha, kwenye mahojiano hayo Jux aliweka wazi kuwa watanzania watarajie albamu mpya kutoka kwake inayoitwa ‘The King of Hearts’.

Leave your comment