Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Jux Zinazovuma 2021

[Picha: Juma Jux Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Juma Jux ni msanii tajika haswa katika mziki wa RnB. Mwaka huu 2021 ameunza vizuri kwa kuachia nyimbo mpya hata kufanya ushirikiano na wasanii wenzake. Hivyo katika nakala hii tunaangazia nyimbo tano ambazo Jux ameachia na kushirikishwa.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia EP Mpya ‘Wanibariki’ Yenye Mziki wa Injili

Mapepe - Juma Jux

Hili ni toleo jipya kutoka wa mfalme wa nyimbo za mapenzi Juma Jux. Katika wimbo huu, Juma anasisitiza kuwa mapenzi hayataki ‘mapepe’, ila utulivu na uaminifu.

https://www.youtube.com/watch?v=G0qRQhNRLcI&ab_channel=AfricanBOY

Sawa - Jux

Sawa’ ni wimbo wake wa kwanza mwaka huu. Juma aliachia wimbo huu kama adhimisho ya mwezi wa mapenzi. Jux anaendelea kuweka wazi kuwa upendo anaouhisi ni mkubwa sana ila tu hajui vile ya kufanya maamuzi yake.

https://www.youtube.com/watch?v=QrLJcXUt7YU&ab_channel=AfricanBOY

Lala – Rayvanny ft Jux

Huu ni wimbo ulio kwenye albamu ya Rayvanny na umepata umaarufi zaidi kwa sababu ya maudhui yake. Katika wimbo huu, Rayvanny na Jux wanazungumzia mapenzi yao ya awali. Wawili hao wameonyesha ubabe kupitia sauti zao.

https://www.youtube.com/watch?v=kSZxCkxUQzo&ab_channel=Rayvanny

Blessings- Abbah ft Jux

Wimbo huu unaelezea jinsi mtu anahisi kubarikiwa kuwa na mwanamke wake. Kanda hii ilielekezwa na Denden na Inno. Wimbo huo ulitengenezwa na kutungwa Abbah Process na upo kwenye albamu yake mpya ‘The Evolution.’

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Wimbo Mpya wa Mapenzi ‘For You’

https://www.youtube.com/watch?v=nK1GTXSMtOc&ab_channel=Abbah

Fashion Killa ft Singah

Ni wimbo unaolezea hisia za Jux na singah kwa binti mrembo na mwana mitindo mwenye ubunifu wa kuvalia nguo za kuvutia. Katika kanda ya wimbo huu mwanabiashara Wolper ameshirikishwa.

https://www.youtube.com/watch?v=99ObsJsQpkw&ab_channel=AfricanBOY

Leave your comment