Nyimbo Mpya: Marioo Aachia Wimbo Mpya wa Mapenzi ‘For You’

[Picha: Marioo Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka nchini Tanzania Marioo ameachia wimbo mpya wa mapenzi kwa jina ‘For You’.

Katika wimbo huu, Marioo anaangazia furaha yake ya kupata sababu ya kuishi kwa sababu ya mapenzi.

Soma Pia: Marioo Ranks Aslay Third Best Bongo Artist after Diamond and Alikiba

Anaanza wimbo huu kwa kushangaa mbona ni mpaka sasa ndio ametambua kuwa dunia ina mazuri.

“Hii dunia kumbe tamu, nilikua wapi kuenjoy wanadamu, yaani dunia kumbe tamu nilikua wapi mmhh, unanipatia mama, nilishaaga li asana na kujikatia tama ulalale…..” hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huu.

Download Marioo Music for Free on Mdundo

Kwa muda mwingi, Marioo amefanya mziki wa mapenzi huku akiangazia masononeko yanayoletwa na kuwa ndani ya mapenzi. Ila leo katika wimbo wa ‘For You’, Marioo yuko radhi kumuimbia mpenzi wake ambaye amempa sababu ya kufurahi maisha.

Soma Pia: How Marioo Missed Out on Sho Madjozi’s ‘John Cena’ Hit

Ngoma hii ni kazi yake ya kwanza mwaka huu na kweli Marioo ameanza kwa uzuri na furaha.

Mdundo wa wimbo huu unafananishwa na ule wa kizomba hivyo unasababu ya kucheza na mpenzi wako.

Maandalizi ya wimbo huu umefanywa na producer tajika kwa jina Producer Abbah huku mchanganyio wa mdundo ukifanywa na Mixkiller.

Wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube huku kanda ya wimbo huu ikitarajiwa hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=0fsh2XkqWcw&ab_channel=MariooOfficial

Leave your comment