Nyimbo Mpya: Nandy Aachia EP Mpya ‘Wanibariki’ Yenye Mziki wa Injili

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Jiunge Nasi Kwenye Telegram

Msanii wa bongo Nandy ameachia EP mpya ya nyimbo za injili kwa jina ‘Wanibariki’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video Mpya ‘Leo Leo’ Akimshirikisha Koffi Olomide

‘Wanibariki’ ni EP iliyo na nyimbo tano za kuabudu na kumshukuru Mungu kwa baraka. Ameachia EP hii kama zawadi kwa mashabiki wake waliotamani afanye nyimbo za injili baada ya kufanya cover wimbo wake Angel Bernard ‘Nikumbushe’ miaka mitatu iliyopita.

Soma Pia: Pakua Mixtape 5 Bora za Nyimbo za Injili

EP yake ina nyimbo kama vile:

Wanibariki

Huu ni wimbo amboo Nandy anaangazia safari yake ya maisha na kumshukuru Mungu kwa baraka alizomjalia. Anaimba na kusema ni Mungu tu amefanya hatetemeki.

Umenifaa

Huu ni wimbo unaelezea namna Mungu amekua mtetezi katika maisha yake. Anaelezea jinsi mambo ya dunia yamekua mazito ila Mungu alijionyesha na kumsaidia haswa katika wakati wa shida.

Download Nandy Music for Free on Mdundo

Nipo Naye

Huu ni wimbo wa maombi ya mwanamke anayemshukuru Mungu kwa kuwa sehemu ya maisha yake kila wakati. Kwa kutomkatia tamaa kwa sababu ya njia zake za dhambi, anamsifu Mungu kwa kumpa kila wakati nafasi nyingine ya maisha.

Asante

Huu ni wimbo wa shukrani na kusifia Mungu kwa kumtendea mema katika nyakati zote.

Noel Song

Huu ni wimbo wa Krismasi unaosifu kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Ni wimbo unao imbwa na Wakristo ulimwenguni kwote haswa siku ya kuzaliwa kwake Yesu. Katika wimbo huu Nandy, kaandika mistari yake katika Kiswahili kwa ufasaha wa hali ya juu.

Mashabiki wanatumai Nandy ataachia Kanda ya nyimbo hizi hivi karibuni.

Leave your comment