Nyimbo Mpya: Nandy Aachia Video Mpya ‘Leo Leo’ Akimshirikisha Koffi Olomide

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Tumia Rafiki Kwenye WhatsApp

Mwimbaji wa Tanzania Nandy hatimaye ameachia vide ya wimbo ‘Leo Leo’ aliomshirikisha msanii nguli kutoka Congo Koffi Olomide.

Wimbo huo una mdundo mzuri ulio na mchaganyiko wa Lingala na bongo. Wimbo huu umetayarishwa na Kimambo na unaangazia maudhui ya mapenzi kati ya watu wawili wanaochanganywa na mpenzi wao.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Kumi Bora Tanzania Februari 2021

“My sweet coco, Penzi kidani nitunzie, Nakesha popo, Kulinda vidanga visiibie, Nadeka mwali, ka motto, Nidekeze mie, baikoko, Mi wa halali, Chanda chema mie…” hii ni baadhi ya mistari ya wimbo huu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mimi Mars Aaachia Video Mpya ‘Wenge’

Nandy na Koffi Olomide kwa kina walifanya kazi nzuri katika uimbaji wao. Kanda hii nayo ina uzuri wake kuanzia kwa maavazi walionayo na densi.

Kinachodhihirika hapa ni kuwa Nandy alitimiza ahadi yake kwa mashabiki kwa kuachia mziki huu wa kufana.

Ukitazama video hii tunaona maonyesho ya nguo za mitindo mbali mbali ikiwemo na ujuzi mkubwa wa wasakataji wa densi.

Download Nandy Music for Free on Mdundo

Koffi Olomide kwa upande wake amekuwa kielelezo kizuri huko Tanzania kwa ajili ya ushirikiano wake na Nandy na hata wa awali na Diamond Platnumz.

Kanda ya wimbo wa ‘Leo leo’ imetengenezwa na Director Elvis huku ikipokewa kwa kishindo.

Kufikia sasa video hii imepata watazamaji zaidi ya elfu themanini na nne.

https://www.youtube.com/watch?v=_8rFTFKMjNU

Leave your comment