Nyimbo Mpya: Mimi Mars Aaachia Video Mpya ‘Wenge’

[Picha: Mimi Mars]

Mwandishi: Branice Nafula

Msanii wa Bongo Mimi Mars ameachia videoyake mpya kwa jina ‘Wenge’.

‘Wenge’ ni wimbo wa kuangazia mrembo mmoja anavyopagawishwa katika upendo. Hivyo Mimi Mars anasema kwa kuwa amepata mapenzi ya kweli na itambidi apunguze ‘Wenge’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Kumi Bora Tanzania Februari 2021

‘Wenge’ ni neno la Kiswahili linalohusishwa na watu ambao hawawezi kutulia mahali moja. Katika muktadha wa wimbo huu ‘Wenge’ ni wimbo unaohusishwa na hulka inayoachwa.

“Ua la moyo limeshachelewa, Furaha yangu wewe na unajua,Ninapokupenda wee,Kama roho yangu,Popote nitapokwenda,Uwe pembeni yangu…” hii ni baadi ya mistari ya wimbo huo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Christina Shusho Aachia Video Mpya ‘Hesabu’

Kanda hii imetengazwa kwa ujuzi wa hali ya juu sana huku Mimi Mars akiendelea kuonyesha uzuri wa upendo.

Mdundo wa wimbo huu umetengezwa na mwandalizi mashuhuri S2kizzy na kufanyiwa mandalizi ya ziada na Ayo Lizer wa Wasafi.

Download Mimi Mars Music for Free on Mdundo

Kwa muda mrefu, Mimi Mars amekua katika fani ya mziki huku akiongezea na kazi ya uigizaji.

 Hivyo ‘Wenge’ ni kazi yake ya kwanza rasmi mwaka huu 2021. Mashabiki wake huku wanatarajia kazi zaidi kutoka kwake.

Kufikia sasa ‘Wenge’ ni wimbo unaondelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube ikiwa imetazamwa na watazamaji zaidi ya elfu kumi na nne.

https://www.youtube.com/watch?v=ZGVxGjGp7Gg&ab_channel=MIMIMARS

Leave your comment