Stamina Aweka Wazi Tarehe na Jina la Albamu Yake Mpya

[Picha: EATV]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Hatimaye rapa kutokea nchini Tanzania Stamina ameanika dhahiri shahiri jina la albamu yake pamoja na tarehe rasmi ambayo ataiachia albamu hiyo.

Stamina ambaye pia ni mmoja wa wanamuziki wanaounda kundi la Rostam ameweka wazi kuwa albamu yake ijayo itaitwa ‘Paradiso’ na imesheheni nyimbo 16. Kati ya hizo, tayari mbili zimeshatoka.

Soma Pia: Diamond Aweka Rekodi Mpya YouTube Baada ya Kupata Watazamaji Bilioni Moja Nukta Tano

Aidha, msanii huyo kupitia akaunti yake ya Instagram ameweka wazi kuwa albamu yake itatoka Oktoba 24 na itakuwa ni albamu yake ya pili tangu aanze kufanya muziki baada ya albamu yake ya kwanza "Mlima Uluguru" iliyotoka mwaka 2015.

"Tarehe 24/10/2021! ndio siku rasmi nitakayotoa album yangu ya pili katika maisha yangu ya mziki. Album inaitwa Paradiso Ina nyimbo 16 nyimbo 2 ambazo zilishatoka nyimbo 14 zote ni mpya hazijawahi kusikika popote. Sijisifii ila ni Album bora kabisa sababu nimeifanya kwa ubunifu na uwezekaji mkubwa mkubwa wa maarifa kwa lengo la kuelelimisa zaidi na kuonyesha nguvu ya kipaji nilichonacho" aliandika msanii huyo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Tanzania na Harmonize, Rich Mavoko, Mabantu na Mr Blue

Stamina anaingia kwenye orodha ya wasanii ambao wapo mbioni kuachia albamu wasanii wengine ni pamoja na Diamond Platnumz, Harmonize, Marioo, Alikiba, Young Lunya na wengineo wengi.

Leave your comment