Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Tanzania na Harmonize, Rich Mavoko, Mabantu na Mr Blue

[Picha: The Star]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Soko la muziki nchini Tanzania linaendelea kuchangamka kwani wasanii tofauti tofauti wanaendelea kuachia bidhaa mpya ambazo bila shaka zinaburudisha na kufanya mashabiki kuzizima kwa furaha.

Soma Pia: Harmonize Atangaza Ujio wa Konde Gang Radio na TV

Hizi hapa ni orodha ya nyimbo mpya ambazo zimeachiwa nchini Tanzania kwa kipindi cha wiki hii.

Mazima - Barakah The Prince

Kwenye wimbo huu, Barakah anaonesha ni kwa namna gani yuko na furaha kwemye mahusiano yake na anamshukuru mpenzi wake kwa dhati sana kwa namna ambavyo anampenda na kumzingatia.

https://www.youtube.com/watch?v=dx9FpQAxkqo

Teacher - Harmonize

Mwalimu mkuu wa muziki wa Amapiano nchini Tanzania Harmonize ameendelea kuonesha ufundi wake kwenye muziki huo baada ya kuachia ‘Teacher’.  Kwenye kibao hiki, Tembo ameongelea masuala kama kiki za kwenye muziki, kuigwa na washindani wake na amenogesha zaidi wimbo huu baada ya kuimba kwa lugha ya kimakonde kwenye aya ya pili.

https://www.youtube.com/watch?v=mPVoKSc6LJo

Sina Shida Nae - Mabantu

Wimbo huu umetayarishwa na Huture ambaye ameshirikiana na Gachi B. Kufikia sasa umetazamwa mara laki moja kumi na nne kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=4p9Mjo7w6x8

KO - Mr Blue

Kwenye ‘KO’, Blue anarudi kwenye misingi ya Hip-hop kwa kujisifia huku akionesha ni kwa namna gani yeye ni mwamba kwenye muziki wa Hip-hop. Kufikia sasa, KO imeshatazamwa takriban mara elfu hamsini na tatu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=UxEHifCMeHQ

Ndo Maana - Rich Mavoko

Wengi humtambua kama Messi wa Bongo Fleva na bila shaka kibao chake kipya ‘Ndo Maana’ kinathibitisha kuwa Rich Mavoko ni kama Messi akiwa uwanjani. Kwenye wimbo huu, Rich Mavoko anaelezea namna gani ambavyo mapenzi yanamuumiza na kumfanya awe mpweke kiasi cha kusikia baridi hasa nyakati za usiku.

https://www.youtube.com/watch?v=iitIRSfllj0

Leave your comment