Diamond Aweka Rekodi Mpya YouTube Baada ya Kupata Watazamaji Bilioni Moja Nukta Tano

[Picha: Pulse Live]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya WCB Diamond Platnumz ameweka rekodi mpya kwenye muziki wake baada ya kufikisha watazamaji Bilioni Moja nukta tano kwemye akaunti yake ya YouTube.

Rekodi hii inakuja miezi takribani kumi na minne tangu msanii huyo afikishe watazamaji Bilioni moja kwenye akaunti hiyo ambayo aliianzisha mwaka 2011. Hii inamaanisha kwamba ndani ya miezi 14 tu, Diamond Platnumz amepata kutazamwa mara milioni 500 kwenye akaunti yake.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa Bongo na Wasanii Diamond, Rayvanny, Zuchu na Ibraah

Kitu kilichochangia Diamond Platnumz kufikisha views bilioni moja nukta tano katika akaunti yake ya YouTube ni hulka ya msanii huyo kuweka maudhui tofauti tofauti kwenye akaunti yake kama video za maneno (lyrics videos), dance video, matamasha mbalimbali anayoyafanya, matukio yake akiwa anarekodi nyimbo studio na kila aina ya maudhui.

Soma Pia: Zuchu Adhibitisha Uwepo wa Kolabo Nyingine Baina Yake na Rayvanny

Rekodi hio inamfanya Diamond Platnumz kuwa ndiye mwanamuziki aliyetazamwa zaidi YouTube kuliko mwanamuziki yeyote barani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.

Aidha, Diamond Platnumz ndiye mwanamuziki anayeongoza kuwa na wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao huo wa YouTube kwani kufikia sasa ana wafuasi Milioni 5 nukta tano kwenye mtandao huo.

Kwa upande wa video za muziki zilizopo kwenye akaunti yake, ‘Yope Remix’ inaongoza kutazamwa kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara milioni 164 ikifuatiwa na ‘Inama’ iliyotazamwa mara milioni 95 ikifuatiwa na ‘Waah’ aliyompa shavu Koffi Olomide ambayo imeshatazamwa mara milioni 82.

Leave your comment