Zuchu Adhibitisha Uwepo wa Kolabo Nyingine Baina Yake na Rayvanny

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutokea lebo ya WCB Zuchu amedhibitisha kuwa ngoma mpya ipo jikoni na hivi karibuni ataweza kuwapakulia mashabiki wake. Ngoma hiyo ni kolabo yake na msanii mwenzake tokea lebo ya WCB Rayvanny.

Soma Pia: Ujumbe wa Zuchu Kwa Mashabiki Baada ya Tamasha Lake Kupata Mafanikio

Zuchu alitangaza ujio wa kolabo hiyo kupitia chapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram. Kwenye chapisho hilo, Zuchu pia alimtakia Rayvany siku njema ya kuzaliwa. Aidha, Zuchu hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na ngoma hiyo, hakutaja muda ambao ngoma hiyo itaachiwa, ila aliwaonjesha mashabiki mistari yake.

Kutokana na picha alizoambatanisha na chapisho hilo, kuna uwezakano ya kuwa video ya wimbo hiyo tayari isharekodiwa.

"Happy birthday @rayvanny I cannot wait for our fans to hear our new hit ambayo ni yangu unataka kunidhulumu sababu mi mwanamke," Zuchu aliandika mtandaoni.

Soma Pia: Zuchu Apigiwa Simu na Rais Samia Akiwa Katikati ya Tamasha lake la Zuchu Homecoming [Video]

Hii haitakuwa mara ya kwanza Zuchu kushirikiana na Rayvanny, takriban miezi minane iliyopita Rayvanny alimshirikisha Zuchu katika wimbo wake ulioitwa 'Number One'.

Ngoma hiyo hadi sasa imetazamwa mara milioni arobaini na nne katika mtandao wa YouTube. Mashabiki wamesubiri kwa hamu sana kolabo hiyo ambayo inatarajiwa kutikisa anga za burudani bongo ikizingatiwa kuwa wasanii hawa wawili ni wakubwa sana barani Afrika.

Wote wanafanya vizuri na kila mmoja ana ushawishi mkubwa sana. Bado haijafahamika iwapo kazi hii itakuwa ushiriakiano baina ya lebo ya Rayvanny ya Next Level Music na WCB, au lebo moja tu kati yao ndio itasimama.

Leave your comment