Zuchu Apigiwa Simu na Rais Samia Akiwa Katikati ya Tamasha lake la Zuchu Homecoming [Video]

[Picha: Wasafi Media]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutokea lebo ya WCB Zuchu ameweka rekodi mpya kwenye muziki wake baada ya kupata simu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa anatumbuiza kwenye tamasha lake la Zuchu Homecoming.

Rais Samia alimpigia Zuchu simu akiwa katikati ya tamasha hilo lililofanyika visiwani Zanzibar wikendi hii.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia ‘Naanzaje’

Kwenye mazungumzo hayo mubashara kabisa, Rais Samia alimsifia Zuchu kwa kufanya tamasha kubwa lililovutia watu wengi na kuahidi kuendelea kuwashika mkono vijana wote ambao wanashiriki kujenga uchumi wa nchi.

Upande wa Zuchu alionekana mwenye furaha isiyo kifani baada ya simu hiyo na alitumia mazungumzo hayo kumhaidi Rais Samia kuwa ataendelea kuwa balozi mzuri na kuitangaza sanaa ya Tanzania kimataifa.

Tamasha la Zuchu Homecoming limeonekana kuteka hisia za watu wengi nchini Tanzania kwani lilihusisha wasanii kadha wa kadha kama Lavalava, Queen Darleen, Gigy Money, Mr Blue, Berry Black, Jux na wengineo.

Soma Pia: Nyimbo Tano za Harmonize, Diamond na Rayvanny Zinazotamba Bongo Wiki Hii

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Samia kupiga simu kwenye matamasha ya wasanii kwani Mwezi Juni mwaka huu Rais huyo alimpigia simu Nandy wakati anatumbuiza kwenye tamasha la Nandy Festival lilipofanyika mkoani Dodoma.

Aidha, Diamond Platnumz kwenye tamasha lake la kutimiza miaka 10 pale Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma lililofanyika kwenye mkesha wa mwaka mpya Desemba 30 2019 , tamasha lake lilisimama kwa muda baada ya aliyekuwa rais hayati John Pombe Magufuli kumpigia simu msanii huyo akiwa jukwaani.

https://www.youtube.com/watch?v=dhHVzBIiHm8

Leave your comment