Nyimbo Tano za Harmonize, Diamond na Rayvanny Zinazotamba Bongo Wiki Hii

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Kitu kizuri kuhusu muziki kutokea nchini Tanzania ni kuwa nyimbo nzuri hukaa nafasi za juu tu siku zote kwani mashabiki hupenda kuskiliza muziki mzuri kutoka kwa wasanii wao.

Soma Pia: TBT: Nyimbo Tano Kali Zilizowahi Kutoka Mwezi Agosti

Pamoja na kuwa wasanii wengi wametoa nyimbo wiki hii, hii hapa ni orodha ya nyimbo tano ambazo zinavuma na ambazo zimesikilizwa sana kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzania:

Mang'dakiwe Remix - DJ Obza ft Harmonize and Leon Lee

Kama ilivyokuwa wiki iliyopita Harmonize anaendelea kufanya vizuri na Amapiano yake ya Mang'dakiwe Remix. Video ya wimbo huu imeonesha umahiri wa Harmonize pamoja na wasanii wengine wa Konde gang kama Anjella kwenye kucheza dansi. Bila shaka kama unatafuta wimbo wa kuruka nao club wikiendi hii basi Mang'dakiwe remix ni chaguo sahihi.

https://www.youtube.com/watch?v=EK8y4hcrJyA

Ibraah - Jipinde

Ibraah kutokea Konde Gang amerudi tena! Na tofauti na tulivyomzoea kwenye nyimbo zake za awali, kwenye ‘Jipinde’ Ibraah anateleza kwenye mdundo uliochangamka  huku akimsifia mpenzi wake namna alivyopendeza. Wimbo huu umeweka rekodi mpya kwenye muziki wa Ibraah kwani huko YouTube ulitazamwa mara Milioni moja ndani ya saa 15.

https://www.youtube.com/watch?v=buiRt-we5SI

‘Iyo’ - Diamond Platnumz ft Focalistic, Mapara A Jazz & Ntoshi Gazi

Amapiano ya Diamond Platnumz inaendelea kufanya vizuri kwani kufikia sasa imeshatazamwa mara milioni sita nukta sita kwenye mtandao wa YouTube. S2kizzy kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni alifichua kuwa wimbo huu ulirekodiwa visiwani Zanzibar pia aliweka wazi kuwa Focalistic na Diamond Platnumz wana nyimbo takribani nne ila bado hazijatoka.

https://www.youtube.com/watch?v=UcOSSs3CNQ0

Chawa - Rayvanny & Whozu ft Ntosh Gazi

Muziki wa Amapiano unazidi kushika kasi nchini Tanzania na hii inathibitishwa na wimbo wa ‘Chawa’ ambao ni wa aina yake. S2kizzy ametumia ufundi mkubwa sana kwenye kuanda mdundo wa wimbo huu kwani ametumia ala tofauti tofauti za muziki kama filimbi na nyinginezo kunogesha kazi hii. Kufikia sasa, wimbo huu umeshatazamwa mara milioni  moja nukta moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=OdeLCyEJLuU

Nimegonga Remix - Kayumba ft Marioo

Muziki wa Singeli unazidi kuota mizizi nchini Tanzania kwani kwa siku za hivi karibuni wasaniii wengi wa Bongo Fleva wamefanya aina hiyo ya muziki. Kilichovutia zaidi ni ushirikiano mzuri ulioonekana kwa wasanii hawa na kwa upande wa Marioo hii ni mara yake ya pili kushirikishwa kwenye Singeli baada ya ‘Nakuja Remix’ aliyoshirikishwa na Balaa Mc kufanya vizuri miezi kadhaa nyuma. Kufikia sasa wimbo huu umeshatazamwa mara laki tatu ishirini na tatu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=CKymo-u3C3s

Leave your comment