TBT: Nyimbo Tano Kali Zilizowahi Kutoka Mwezi Agosti

[Picha: Muziki Mpya]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wazungu wanaiita Throw Back Thursday na ni siku maalum ambayo tunaangazia na kujikumbushia matukio ya zamani ambayo kwa namna moja au nyingine yamegusa maisha.

Soma Pia: Ibraah Ajibu Madai ya Kununua Watazamaji wa Wimbo wake ‘Jipinde’ Kwenye YouTube

Katika kuienzi siku hii makala hii inaangazia nyimbo tano kali ambazo wasanii kutokea nchini Tanzania waliziachia miaka ya nyuma ndani ya mwezi wa Agosti.

Soma Pia: Rich Mavoko Azungumzia Kufanya Kazi na Harmonize

Likizo - Aslay

Nani kama Aslay linapokuja kwenye kuimba nyimbo za kubembeleza? Aslay alitoa wimbo wa ‘Likizo’ Agosti 9 mwaka 2017. Kwenye kibao hiki, Aslay anamlilia mpenzi wake aliyemtenda na Aslay anaomba kupewa ‘Likizo’ ya kutokutendwa na mpenzi wake. Kufikia sasa video ya wimbo huu ishatazamwa mara milioni tisa kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=xX6V5bt5yjg

Bugana - Billnass ft Nandy

Ilipofika Agosti 30 mwaka 2019 ndipo Billnass aliamua kutetemesha kiwanda cha muziki nchini Tanzania baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Bugana’ akimshirikisha Nandy. ‘Bugana’ ni wimbo unaosherehekea upendo baina ya watu wawili wanaopendana ambao kupitia kibao hiki wanawekeana ahadi kupeana mapenzi motomoto na kipindi wimbo huu unatoka wengi walitafsiri kama ni majibu ya wawili hao kwa mashabiki zao.

https://www.youtube.com/watch?v=f5Po301yHjM

Pusha - Aslay

Ni miaka minne tu imepita tangu Aslay aachie ‘Pusha’ lakini bila shaka mtayarishaji wa muziki Zest alifanya kazi nzuri kwani wimbo huu bado unaishi hadi leo. Agosti 28 mwaka 2017 ndipo Aslay alipoachia wimbo huu na katika kibao hiki, Aslay anatembea kwenye mdundo wenye vionjo vya reggae huku akimuhadithia ‘Pusha’ jinsi ambavyo kuna kijana anataka ampore mpenzi wake.

https://www.youtube.com/watch?v=qCm1jbjuj9I

Chuma Ulete - Rayvanny

Video ya wimbo huu ilitoka Agosti 6 mwaka 2017 na Rayvanny kwenye wimbo huu analalamika sana kuhusu mpenzi wake ambaye anamuomba sana hela kiasi cha kumfanya kama akose furaha na amani. Kufikia sasa, wimbo huu umetazamwa mara milioni sita nukta moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=JTqCnZU8atY

Niwahi - Rich Mavoko

Messi wa Bongo Fleva Rich Mavoko alitoa ‘Niwahi’ Agosti 7 mwaka 2020 na wimbo huu uliashiria ujio mpya wa Rich Mavoko kwenye kiwanda cha muziki baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu. Pamoja na kwamba ni mwaka umeshapita sasa lakini wimbo huu bado unaonekana ni mpya kabisa masikioni mwa wasikilizaji.

https://www.youtube.com/watch?v=QIiJiJ0X7Vw

Leave your comment