Rich Mavoko Azungumzia Kufanya Kazi na Harmonize

[Picha: Nairobi News]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutokea nchini Tanzania Rich Mavoko ametoa mawazo yake kuhusu kufanya kazi na msanii Harmonize kutokea Konde Gang.

Rich Mavoko ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa ‘Nidonoe’ amesema kuwa yupo tayari kufanya kazi na Harmonize iwapo kutakuwa na makubaliano ya kibiashara baina ya pande zote mbili.

"Mimi naamini ikitokea kwenye business way tunaweza kufanya sababu sisi ni vijana na tunaweza kutengeneza hichi kitu kwa ukubwa," alizungumza staa huyo.

Soma Pia: Khadija Kopa, Jux na Wasanii Wengine Watakaotumbuiza Kwenye ‘Zuchu Homecoming’ [Orodha Rasmi]

 Kwa muda mrefu sasa, mazungumzo juu ya wimbo wa pamoja baina ya wasanii hao wawili yameshamiri kutokana na ukweli kuwa Harmonize na Rich Mavoko walikuwa chini ya lebo ya WCB kisha wakajitoa.

Ikumbukwe kuwa Harmonize pamoja na Rich Mavoko kipindi wapo WCB walishafanya wimbo wa pamoja unaoitwa ‘Show Me’ uliotoka April mwaka 2017 na ni wimbo uliopendwa sana mashabiki. Kufikia sasa, wimbo wa ‘Show Me’ ushatazamwa mara Milioni ishirini kwenye mtandao wa YouTube.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia ‘Jipinde’

Aidha, kwenye mahojiano hayo aliyoyafanya kwenye kituo cha Times FM, Rich Mavoko alipoulizwa kuhusiana na tetesi kuwa tayari ameshafanya wimbo na msanii Alikiba, Rich Mavoko aliweka wazi kuwa bado hajafanya wimbo wowote na msanii Alikiba na tetesi zilizopo hazina ukweli wowote.

Leave your comment