Khadija Kopa, Jux na Wasanii Wengine Watakaotumbuiza Kwenye ‘Zuchu Homecoming’ [Orodha Rasmi]

[Picha: Dar Mya Online TV]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pakua Ngoma Zake Khadija Kopa Bure Kwenye Mdundo

Tamasha la Zuchu Homecoming lililosubiriwa kwa hamu sana na mashabiki limesalia na siku tatu tu kutendeka katika uwanja wa Amani mkoani Zanzibar. Tamasha hilo limeibua joto jingi katika tasnia ya burudani ya Tanzania, huku wadau tofauti wakisubiri kuona mafanikio yake.

Soma Pia: Nyimbo 5 za Khadija Kopa Zilizompa Hadhii Katika Taarab [Video]

Zuchu ni mwanamuziki mwenye ushawishi mkubwa na wafuasi wengi mno. Amesifiwa na wengi kwa jinsi alivyopata umaarufu na mafanikio kimuziki ndani ya muda mfupi sana. Ila wakati wa kujua mbivu na mbichi umewaidia, kwani hili ndilo tamasha lake la kwanza.

Tamasha hilo hata hivyo limevutia wengi kutokana na orodha ya wasanii maarufu watakaotumbuiza jukwaani siku hio kuu.

Baadhi ya wanamuziki watakaokanyaga jukwaani na kufanikisha tamasha hilo ni kama wafuatavyo:

Soma Pia: Khadija Kopa Asimulia Sauti Ilvyompotea Akiwa Jukwaani Akashindwa Kuimba

 • Juma Jux
 • Mr Blue
 • Lulu Diva
 • Gigy Money
 • Chege
 • Baba Levo
 • Queen Darleen
 • Kidene
 • Dula Makabila
 • Fimbo ya Musa
 • Khadija Kopa na wengine wengi.

Tayari baadhi ya wasanii hao wamechapisha ujumbe katika mitandao ya kijamii kudhibitisha kuwa watakuwepo kwenye tamasha hilo.

 "Zanzibar Jumamosi hii let’s support @officialzuchu anarudi nyumbani, tukutane Amani karibuni sana," Juma Jux aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

"Hey God Mother Drill Nipo Hapo tar 21/08/2021 save the date Zuchu Day," chapisho lake Gigy Money mtandaoni lilisomeka.

Hapo awali Zuchu alisema kuwa baadhi ya wasanii walioalikwa kwenye tamasha hilo hawangeweza kufika kwa sababu ya majukumu yao ya kibinafsi.

Leave your comment