Nyimbo 5 za Khadija Kopa Zilizompa Hadhii Katika Taarab [Video]
19 February 2021
[Picha: Khadija Kopa Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Bi Khadija Kopa almaarufu,‘Malkia wa Mipasho’ anasherehekewa kuwa miongoni mwa wanawake wanaojiamini zaidi nchini Tanzania. Bi Khadija Kopa ni msanii mwenye hadhii kubwa sana katika mziki wa Taarab. Anasifika kuwa miongoni mwa wasanii waliofanikisha mziki wa taarab katika kanda ya Afrika mashariki.
Read Also:Taarab Music in Tanzania: Origin, Evolution, Top Artists and Latest Trends
Katika nakala hii, tunaangazia nyimbo zake tano za taarab zilizompa hadhii katika fani hii ya mziki:
Top in Town
Huu ulikua wimbo wake wa kwanza kutoka albamu yake ya ‘Top in Town’. Kwenye wimbo huu, anaelezea kwanini yeye ni bora zaidi kwa wote katika mziki wa taarab. Kufikia sasa, ni wimbo ulio na zaidi ya watazamaji zaidi ya milioni moja na laki tatu kwenye mtandao wa YouTube.
Lady with Confidence
Huu ni wimbo wa kumsifia mwaname mwenye sifa za kipekee. Anaangazia mwanamke wa kujiamini katika maisha. Hapa Kopa alifanya wimbo huu kuwapa wanawake nguvu ya kujiamini.
Full stop
‘Full Stop’ ndio wimbo uliomwongezea hadhi ya “Malkia wa Mivchambo”. Katika wimbo huu, anaangazia namna watu wengine wang’anga’nia kumharibia sifa. Hivyo anawakanya huku akijipa sifa ya kuwa Komando wa kike. Kwenye mtandao wa YouTube, ana watazamaji zaidi ya miliioni moja.
Read Also: 2 Strategies Khadija Kopa is Using to Remain Relevant in Fast-Changing Bongo Music Industry
Mjini Chuo Kikuu
Huu ni wimbo uliona maudhui ya kuhimiza watu kujituma. ‘Mjini Chuo Kikuu’ ni wimbo unaongazia namna watu wanovyoishi mjini wakitafta namna ya kujikimu. Hivyo mjini chuo kikuu ni wimbo wa mafunzo muhimu maishani.
Wigi linawasha
Huu ni wimbo uliopokelewa kwa ukubwa sana. ‘Wigi Linawasha’ limetumika kuonyesha namna kukaa ukifwatilia mambo ya watu si muhimu ila kutafuta hela.Wimbo huu Bi. Kopa aliuachia miaka miwili iliyopita na kufikia sasa bado haina video.
Leave your comment