Khadija Kopa Asimulia Sauti Ilvyompotea Akiwa Jukwaani Akashindwa Kuimba

[Picha: Khadija Kopa Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pakua Ngoma Zake Khadija Kopa Bure Kwenye Mdundo

Mwanamuziki aliyebobea kutoka Tanzania Khadija Kopa amejitokeza na kusimilia tukio lililomfanyikia ambalo kamwe hatolisahau katika safari yake ya muziki. Akizungumza katika mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha Wasafi FM, Khadija Kopa alihadithia jinsi sauti ilimpotea wakati mmoja akiwa jukwaani.

Soma Pia: Khadija Kopa Asheherekea Miaka 25 Katika Tasnia Ya Muziki

Khadija Kopa alisema kuwa siku hiyo alikuwa amepata mwaliko wa kutumbuiza katika hafla ya harusi. Hafla hiyo ilikuwa yenye watu wa hadhi ya juu ikiwemo marais na viongozi wengine wa kuheshimika.

Alipofika kwenye hafla hiyo, Khadija Kopa alikaribishwa jukwaani kuimba ngoma zake za mtindo wa Taarab. Cha kushangaza ni kuwa ghafla sauti ilimpotea Khadija Kopa na akashindwa kuimba. Watu walimshangilia huku DJ akicheza nyimbo zake ila Khadija Kopa hakutokwa na sauti ya kiuimba.

Ilimbidi arudi aketi chini huku yeye mwenyewe akibaki na maswali mengi kichwaani. Hata hivyo, alikaribishwa tena kwa mara ya pili na kwa bahati nzuri aliweza kuimba.

Soma Pia: Nyimbo 5 za Khadija Kopa Zilizompa Hadhii Katika Taarab [Video]

"Tukio ambalo sitaweza kulisahau maishani mwangu nililokutana nalo katika muziki wangu ni kuna siku kulikuwa na shughuli kubwa, harusi kubwa ambayo ilikutanisha viongozi, marais lilikuwa bwawani Zanzibar. Basi mimi nikatangazwa kwenda kuimba, na nilitangazwa niende nikaimbe wimbo wa kadandie. Basi nimekwenda nimefika pale, nimesimama kwenye steji, nimeamkia nmesimama niende nikaimbe basi ikawa sauti haitoki," Khadija Kopa alihadithia.

 Khadija Kopa ni mmoja wa wasanii wakongwe sana katika tasnia ya muziki ya Tanzania na bado anaheshimika kutokana na mchango wake kwenye ukuzi wa muziki wa Taarab.

Leave your comment