Khadija Kopa Asheherekea Miaka 25 Katika Tasnia Ya Muziki

[Picha: Afrika Lyrics]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania Khadija Kopa anasherehekea miaka 25 katika tasnia ya muziki.

Khadija Kopa ameingia katika historia kama mmoja wa wanamuziki wakongwe katika tasnia ya burudani ya Tanzania. Mwanamuziki huyo alifanya hafla ambapo alisherehekea mafanikio hayo pamoja na familia yake na wale walio karibu naye.

Soma Pia: Nyimbo 5 za Khadija Kopa Zilizompa Hadhii Katika Taarab [Video]

Watu wengi katika hafla hiyo walikuwa watoto ambao wana talanta ya kuimba. Katika mahojiano ambayo alifanya wakati wa hafla hiyo, Khadija alielezea kuwa alichagua kuwa na watoto kwenye hafla yake kama njia ya kukabidhi tasnia ya burudani kwa kizazi kipya.

Alisisitiza kuwa ni kizazi kipya ambacho kitahakikisha tasnia ya muziki wa Tanzania inabaki hai hata kwa kuondoka kwa wasanii kama yeye.

Soma Pia: Taarab Music in Tanzania: Origin, Evolution, Top Artists and Latest Trends

Aliongeza zaidi kuwa alikuwa amejijengea urithi zaidi ya miaka 25. "Baada ya miaka 25 wazungu walisema unaanza kujenga urithi wako. Na kama tunataka tasnia ikue lazima tuanze kuwashirikisha watoto ambao tunawapata sisi vijiti. Ndio maana nikaamua sherehe itaendelea iwapo Mungu atanipa afya ya mzima," Khadija Kopa alisema.

Khadija Kopa pia ni mama wa staa wa muziki wa Tanzania Zuchu. Zuchu amekua mmoja wa wanamuziki wa Kitanzania wenye ushawishi mkubwa na amesainiwa kwa lebo ya rekodi ya muziki ya WCB.

Leave your comment