Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia ‘Jipinde’

[Picha: Ibraah Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka lebo ya Konde Music Worldwide Ibraah ameachia wimbo mpya wenye jina ‘Jipinde’.

Tofauti na tulivyomzoea kwenye nyimbo zake za awali kama ‘Mapenzi’, ‘Wa Ndoto’ na hata ‘Nani’, ndani ya kibao hiki, Ibraah anapindua meza kwa kutuonesha namna ambavyo anafurahia mahusiano yake ya sasa na kwa namna gani anampenda na kumthamini mpenzi wake.

Soma Pia: Rosa Ree Kuwakutanisha Frida Amani, Chemical Ndani ya Ngoma Moja

"Shida ya upendo uko moyoni natamani nikuoneshe ila hauonekani we my sweet my hani bani nimependa kweli sio kuhaving fun," anaimba Ibraah kwenye aya kwanza ya wimbo huu.

Kuonesha kuwa Ibraah amerudi kiutofauti, Bboy Beats ambaye ndiye amehusika kutayarisha wimbo huu ametengeneza mdundo wa kuchangamka unaoenda sawia na melody ya Ibraah.

 Ni vyema kuweka wazi kuwa hii si mara ya kwanza kwa Bboy na Ibraah kufanya kazi pamoja kwani wawili hao washafanya kazi kwenye wimbo wa ‘Nitachelewa’ uliotoka mwaka jana.

Soma Pia: Amber Lulu Alalamika Kutoshabikiwa Kama Wasanii Walio Kwenye Lebo Tajika Tanzania

Kando na Ibraah, Bboy amehusika kutengeneza ‘Nobody’ pamoja ‘Kama’ za msanii Anjella.

Video ya wimbo huu imeshatazamwa mara elfu sitini na tano kwenye mtandao wa YouTube.

Ndani ya miezi miwili bila kutoa wimbo, Ibraah amekuwa akidokeza miradi yake kadhaa ambayo ipo jikoni kwani ilipofika Juni 21, kupitia akaunti yake ya Instagram alidokeza kuna albamu inakuja.

Julai 24 pia Country Wizzy pamoja na Ibraah walionekana kwenye video fupi wakiwa studio na Bboy wakitayarisha ngoma ya pamoja.

https://www.youtube.com/watch?v=qa7tp22NV8o

Leave your comment