Amber Lulu Alalamika Kutoshabikiwa Kama Wasanii Walio Kwenye Lebo Tajika Tanzania

[Picha: Amber Lulu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu nchini Tanzania Amber Lulu amelalamikia kutoshabikiwa kisa hayupo kwenye lebo ya kurekodi kama wenzake. Katika taarifa aliyochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Amber Lulu alidai kuwa nyimbo zake hazipati watazamaji ikilinganishwa na wasanii wengine waliosaniwa katika lebo zenye majina ya kutajika.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia ‘Yalaaaa’

Kulingana na Amber Lulu, wasanii waliopo kwenye lebo za kutajika wanapata idadi kubwa ya watazamaji licha ya kutoa nyimbo zenye ubora wa chini. Alieleza kuwa kwa sababu yeye ni msanii huru, hapati wafuasi wengi licha ya kuachia ngoma nzuri zenye ubora wa hali ya juu.

"Nimekaa nimesikiliza nyimbo zenuuu za amapiano lakini hiiii ni nomaaaaaaa #AMAPIANOQEEN Utopolo tu Sema mnabana sana amapiano azielewek mnazipa air time cjui mnatuchukulia powa watu tunaangaika kisa et watu wapo Lebel flan bhas vituu vyetu kisa tunajipambania atuna Lebel mnatuona ma b**** tuu mnaishia kutusifia kifala unajua kuimba unajua kuimba tunajishushaaa mpka tunachokaaa," Amber Lulu aliandika mtandoni.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Mpya Zilizoachiwa na Rayvanny, Jux, Marioo na AY

Aidha, Amber Lulu alitoa mfano wa wimbo wake wa ‘Una Shingapi’ ambao aliuachia mapema mwaka huu. Ngoma hiyo kufikia sasa iko na takriban watazamaji laki mbili, jambo ambalo halijamfurahisha msani huyo.

"Nyimbo imetoka mwezi 7 sasa eti ina views 240k Jaman. Izo nyimbo zao mbovuu sasa et one day 1 gafla milion 2. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni Halafu hapo hapo et wasanii tumieni uwezo wenu msinunue maroboti kwa mtindo huuu," alisema Amber Lulu.

Leave your comment