Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Mpya Zilizoachiwa na Rayvanny, Jux, Marioo na AY

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Nchini Tanzania mambo yanaendelea kuwa sukari kwenye kiwanda cha muziki maana wiki hii wasanii tofauti tofauti wametoa nyimbo nzuri ambazo zimekosha sana mashabiki. Zifuatazo ni ngoma mpya zilizoachiwa Tanzania wiki hii:

Soma Pia: Video za Diamond, Mbosso, Harmonize na Alikiba Zinazotamba Bongo Wiki Hii

Chawa - Rayvanny & Whozu ft Ntosh Gazi

Baada ya Ntosh Gazi kufanya kazi nzuri kwenyengoma ya ‘Iyo’ ilioachiwa na Diamond,  ikabidi Rayvanny na Whozu wamuite wafanye wimbo huu unaoitwa ‘Chawa’.  Wimbo huu uliotayarishwa na S2kizzy una mahadhi ya Amapiano. Kufika sasa video ya wimbo huu imetazamwa mara laki nane na elfu tatu kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=OdeLCyEJLuU

Nimegonga Remix - Kayumba ft Marioo

Kayumba anaungana na Marioo kutupa muziki halisiw a Singeli. Wimbo huu umetayarishwa na Jay Stereo huku Majagi King akihusika kwenye kuandaa video. Video ya wimbo huu ishatazamwa mara laki moja themanini kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=CKymo-u3C3s

Pakua Nyimbo za Marioo Bure Kwenye Mdundo

Jimmy Chansa ft Jux - Fahamu

Kama unatafuta wimbo mzuri wa mapenzi kwa ajili ya mpenzi yako basi Jimmy Chansa na Juma Jux wametimiza hilo kupitia wimbo wao mpya ‘Fahamu’. Wimbo huu umefumwa na mashairi mazuri na kwenye aya ya kwanza Jux anaimba kwa kutumia sauti yake iliyotaradadi. Video ya wimbo huu imeongozwa na Director Ivan na kufikia sasa imeshatazamwa mara laki moja thelathini kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=86NFZihbQBs

Sambaloketo - Jay Melody

Wimbo huu unamzungumzia namna ambavyo Melody amezama kwenye penzi zito akiwa na mwanandani wake. Mdundo wa kibao hiki umetayarishwa na  Mr LG ambaye ni mojawapo kati ya watayarishaji muziki makini sana hapa nchini Tanzania. Kufikia sasa wimbo huu umetazamwa mara laki moja thelathini na moja kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=D8ElsB5Sr2Y

Stakaba - AY ft Mimi Mars

 Nguli wa muziki wa Hip-hop nchini Tanzania AY anarudi tena kwenye kiwanda cha muziki lakini kwa sasa harudi peke yake bali anaungana na Mimi Mars kwenye wimbo mpya ‘Stakaba’. ‘Stakaba’ ni wimbo wa mapenzi na unamuonesha AY na Mimi Mars wakivaa uhusika wa wapenzi ambao wanafurahia penzi lao na bila shaka muunganiko wa wasanii hawa wawili umeweza kuburudisha sana mashabiki kwenye wimbo huu.

https://www.youtube.com/watch?v=qvtiVJ5fWbY

Leave your comment