Video za Diamond, Mbosso, Harmonize na Alikiba Zinazotamba Bongo Wiki Hii

[Picha: Citi Muzik]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Imekuwa ni wiki ya harakati sana kwenye kiwanda cha muziki Tanzania pamoja na kwamba wasanii wengi wakubwa kwa wadogo wametoa nyimbo huku lebo kubwa tatu nchini Tanzania WCB, Konde na Kings' Music zikiendelea kutawa.

Soma Pia: Nyimbo Mpya : Rayvanny Aungana na Whozu, Ntoshi Gazi Kuileta ‘Chawa’ [Video]

Hii hapa orodha ya nyimba tano zinazovuma Tanzania kwenye YouTube:

Mang'dakiwe Remix - Dj Obza, Harmonize & Leon Lee

Bosi wa Konde Gang Harmonize anashikilia usukani wiki hii na Amapiano hii akiwa na Dj Obza pamoja na Leon Lee. Video ya Mang'dakiwe Remix imeongozwa na Director Chris na kufikia imeshatazamwa mara Milioni 2 nukta tatu kwemye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=EK8y4hcrJyA

Iyo - Diamond Platnumz ft Focalistic, Mapara A Jazz & Ntoshi Gazi

Muziki wa Amapiano unaendelea kupamba moto hapa nchini Tanzania kwani ‘Iyo’ inazidi kufanya vizuri. ‘Iyo’ imeshatazamwa mara milioni tano nukta sita kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=UcOSSs3CNQ0

Jealous - Alikiba ft. Mayorkun

Wimbo wa ‘Jealous’ unaendelea kupamba moto nchini Tanzania kutokana na mashairi mazuri yaliyopamba kibao hiki ambacho kimeachiwa wiki chache zilizopita. Kufikia sasa, video ya wimbo huu imetazamwa mara Milioni 6 nukta nne kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=LQyCY1t--GU

Tulizana - Mbosso ft Kilimanjaro Band

Mwanamuziki Mbosso anaendelea kupeperusha vyema bendera ya WCB baada ya kuachia video yake ya ‘Tulizana’ Agosti 7 mwaka huu. Kwenye video ya ‘Tulizana’, Mbosso anathibitisha kuwa penzi linaweza kuchipua popote kwani video hii inamuonesha Mbosso akiwa kwenye mazingira ya kijijini akiwa amezama kwenye penzi zito na binti ambaye ana wazazi wakali. Kufikia sasa, ‘Tulizana’ imeshatazamwa mara laki nane sitini na saba kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=kP1Awx00FJc

 Your Love - Mbosso ft Liya

Kwenye kibao hiki, Mbosso anakutana na mwanamuziki kutokea Nigeria Liya ambaye ameweza kuimba vizuri kwa lugha ya kiswahili kwenye wimbo huu. Mpaka sasa, video hii imeshatazamwa mara laki saba arobaini na tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=-2Wpm87d2nE

Leave your comment