Nyimbo Mpya : Rayvanny Aungana na Whozu, Ntoshi Gazi Kuileta ‘Chawa’ [Video]

[Picha: Lite9ja]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa lebo ya Next Level Music Rayvanny ameungana na Whozu kwenye wimbo mpya uitwao ‘Chawa’ wakiwa wamemshirikisha msanii kutokea nchini Afrika Kusini Ntoshi Gazi.

‘Chawa" ni wimbo unaofuata miondoko ya Amapiano na bila shaka wimbo huu unategemewa kukita sana kwenye klabu na sehemu mbalimbali za starehe ndani na nje ya Tanzania.

Soma Pia: Zuchu Amsifia Kidene na Kumkaribisha Kwenye Tamasha la Zuchu Homecoming

Nguli wa muziki nchini s2kizzy amehusika katika kutayarisha wimbo huu. Kama ilivyokuwa kwenye ‘Iyo’, S2kizzy ametengeneza mdundo wenye nguvu na ulioongezwa na ala tofauti tofauti za muziki kama filimbi.

Akumbukwe kuwa Ntoshi Gazi alikuwa ni mojawapo ya wasanii walioshirikishwa kwenye wimbo wa ‘Iyo’ wa Diamond Platnumz na wimbo huu ni wa kwanza kutoka kwa Rayvanny na Whozu kufanya Amapiano.

Soma Pia: Stamina Atangaza Kuachia Albamu kwa Kumbukumbu za Mamake

Aidha video ya wimbo huu imeongozwa na Eris Mzava ambaye pia amefanya kazi kwa video zingine za Rayvanny kama vile; ‘Sugu’, ‘Jeniffer remix’ pamoja na ‘Number One remix’ akiwa na Enisa.

Video ya ‘Chawa’ imepambwa na miondoko mbalimbali ya dansi huku mzava akitumia ufundi mkubwa sana kwenye kuchagua mandhari mazuri ya video.

Video hii imeonesha maisha Whozu na Rayvanny wanavyoweza kubadilisha mitaa kuwa sehemu ya kucheza dansi. Kufikia sasa, video ya wimbo huu imeshatazamwa mara laki moja sitini na tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=OdeLCyEJLuU

Leave your comment