Stamina Atangaza Kuachia Albamu kwa Kumbukumbu za Mamake

[Picha: Stamina Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Stamina ametangaza tarehe rasmi ambayo ataachia albamu yake. Katika ujumbe, aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii, Stamina alifichua kuwa albamu hiyo ameifanya kwa kumbukumbu za marahemu mamake.

Soma Pia: Rosa Ree Atangaza Kukamilisha Albamu Yake

Albamu ya Stamina itaachiwa tarehe 24 mwezi wa 10 mwaka huu. Tarehe hiyo pia ndio siku ambayo mamake Stamina alifariki na hivyo basi uzinduzi wa albamu hiyo utakuwa kwa kumbukumbu zake.

Stamina alidhibitisha katika chapisho lake kuwa utengenezaje wa albamu hiyo ushakamilika na kilchosalia kwa sasa ni kuiachia tu. Stamina hata hivyo alikuwa makini kutofichua habari zaidi kuhusiana na albamu hiyo. Hakutaja idadi ya wimbo itakayokuwa kwenye albamu au majina ya nyimbo zitakazokuwepo pia.

Soma Pia: Harmonize Afunguka Kuhusu Video Iliyomwonyesha Kajala Akiburudika na Wimbo wa ‘Sandakalawe’

"Album is done!,Confirmed 24/10/2021 inatoka rasmi,siku ya kumbukumbu kwangu...sababu ni siku aliyofariki marehemu mama yangu!" chapisho la Stamina mtandaoni lilisomeka.

Mashabiki walijitokeza na kumpongeza Stamina kwa kukamilisha albamu yake. Wengine pia walimtia moyo kuhusiana na kumbukumbu ya marehemu mamake. Stamina kwa sasa ameingia katika orodha ya wasanii wakubwa wa bongo ambao wanatarajiwa kuachia albamu zao.

Wengine waliopo kwenye orodha hiyo ni pamoja na Harmonize, Alikiba na Diamond. Hizi ndizo baadhi ya albamu ambazo zinasubiriwa kwa hamu sana Tanzania.

Wasanii wengine ambao waliachia albamu zao hivi maajuzi ni pamoja na Ben Pol na Nandy. Nyimbo zilizo kwenye albamu zao zimepokelewa vizuri na mashabiki.

Leave your comment