Harmonize Afunguka Kuhusu Video Iliyomwonyesha Kajala Akiburudika na Wimbo wa ‘Sandakalawe’

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki chache zilizopita wimbo wa ‘Sandakalawe’ kutoka kwake Harmonize ulivuma sana mtandaoni. Ngoma hiyo ilipata umaarufu miongoni mwa mashabiki wa Harmonize.

Gumzo hata hivyo iliibuka mtandaoni baada ya Kajala ambaye ni mpenzi wa zamani wa Harmonize kuonekana akiimba ngoma hiyo akiwa sehemu ya burudani.

Baadhi ya mashabiki waliachwa na mshangao huku wengine wakimpongeza Kajala kwa kumuunga mkono Harmonize kimuziki licha ya tofauti zao za kibinafsi.

Soma Pia: Rayvanny Apata Mafanikio Makubwa na Ngoma Yake Mpya ‘Patati Patata’

Harmonize kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu video hiyo ya Kajala iliyovuma sana mtandaoni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize alichapisha video hiyo na kuambatanisha ujumbe wa maelezo.

Harmonize alifichua kuwa Kajala alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuuskiza wimbo wa ‘Sandakalawe’ baada ya kurekodiwa. Alisema kuwa tangu mwanzo kabla ata ya ngoma hiyo kuachiwa , Kajala alikuwa ameupenda. Hivyo basi haikuwa jambo la kushangaza kumwona akiburudika na ngoma hiyo licha ya hao kutofautiana.

Soma Pia: S2kizzy: Diamond Ana Zaidi ya Collabo Tatu na Wizkid

"Meet my big sister #Kajala on her best mood. Let her love the pure music ukimuangalia kwa ndani kabisa kuna machozi ya furaha kwasababu hiii ngoma aliipenda day one ...! By the way yeye alikuwa wakwanza kuisikiza baada tu yaku record usiku wa manane ...!!!!! so lovely and she was a bit tips," chapisho la Harmonize mtandaoni lilisomeka.

Kwa sasa Harmonize ameteka anga za burudani na wimbo wake wa ‘Mang'dakiwe’ aliouachia hivi karibuni kwa ushirikiano na wanamuziki wa Afrika Kusini DJ Obza na Leon Lee.

 

Leave your comment