Rayvanny Apata Mafanikio Makubwa na Ngoma Yake Mpya ‘Patati Patata’

[Picha: Rayvanny Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkuregenzi mkuu wa Next Level Music (NML) Rayvanny bila shaka ni mmoja wa wasanii kutoka Tanzania wanaojituma sana. Bidii yake imemfanya kuandikisha rekodi kimuziki kila kuchao na pia kuongeza idadi ya mashabiki wake nje ya Tanzania.

Soma Pia: Remix Tano Kali Zilizoachiwa na Rayvanny

Siku chache zilizopita Rayvanny alisafari kuelekea Zimbambwe kwa kazi ya muziki. Safari hiyo ilitokea muda mfupi tu baada ya yeye kumkaribisha msanii wa Nigeria Guchi nchini Tanzania kwa minajili ya kolabo.

Baada ya safari yake ya Zimbambwe iliyokumbwa na ukimya sana, Rayvanny alirudi Tanzania. Mnamo tarehe nne mwezi Agosti ngoma ambayo Rayvanny pamoja na Koffi Olomide walikuwa wameshirikishwa na msanii wa Zimbambwe Roki iliachiwa. Ngoma hiyo ilivuma na kupata watazamaji wengi sana.

Soma Pia: Nyimbo Mpya:Ngoma 5 Zilizoachiwa Bongo na Rayvanny, Marioo na Barakah the Prince

Muda mfupi tu baada ya kuachiwa tayari ilikuwa imeshikilia nambari moja katika orodha ya nyimbo zinazovuma sana katika mtandao wa YouTube nchini Zimbambwe. Cha kufurahisha hata zaidi ni kuwa ngoma hiyo iliyopewa jina ‘Patati Patata’ ilishikilia nafasi ya pili katika ngoma zinazovuma YouTube nchini Afrika Kusini.

Mafanikio hayo yalimfanya Rayvanny kuwa miongoni mwa wasanii wachache sana kutoka bongo ambao kazi zao zimevuma kiasi ya kuwa nambari mbili YouTube Afrika Kusini.

Rayvanny katika ujumbe aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram aliwashukuru mashabiki wake na pia mwelekezi wa filamu Director Kenny aliyeshughulikia video ya ngoma hiyo.

"Msanii wa kwanza Tanzania kua namba 2 on trending #SouthAfrica#chui number 2 on trending in #SouthAfrica mwanangu @director_kenny unazifanyaga nini hizi video," Rayvanny aliandika mtandaoni.

Leave your comment